Olimpiki ya Walemavu: Lauritta Onye aipa Nigeria medali ya dhahabu katika mchezo wa kurusha kitufe
Lauritta Onye ameishindia Nigeria medali ya dhahabu katika mchezo wa Shotput kwa upande wa wanawake katika Michezo inayoendelea ya Olimpiki ya walemavu nchini Brazil.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Onye aliweka historia kwa kuipa nchi yake medali hiyo ya kwanza lakini pia kuweka rekodi mpya ya dunia baada ya kurusha kitufe kwa umbali wa Mita 8.40.
Nigeria sasa ni ya 10 duniani na ya kwanza barani Afrika kwa medali 9, Sita za dhahabu, Mbili za fedha na Moja ya shaba.
Nafasi ya pili ilimwendea Rima Abdelli raia wa Tunisia aiyejishinda medali ya fedha huku Lara Baars kutoka Uholanzi akishinda medali ya shaba.
Jedwali la Medali
Dhahabu Fedha Shaba Idadi
- China 50 40 28 118
- Ungereza 28 16 19 63
- Ukraine 22 19 20 61
- Marekani 16 17 13 46
- Brazil 9 17 9 35
- Australia 7 13 14 34
- New Zealand 7 3 3 13
- Uholanzi 6 8 12 26
- Uzbekistan 6 4 13 23
- Nigeria 6 2 1 9