Pata taarifa kuu
TENESI

Federer asema anajiandaa na Australian Open mwakani, kutoshiriki US Open

Mchezaji tenesi rais wa Uswis, Roger Federer amesema hivi sasa analenga kujiimarisha na kujiweka tayari kwa mashindani ya mwakani ya Australian Open, baada ya kujikuta akiwa nje ya uwanja kutokana na majeraha aliyoyapata katikati ya msimu wa mwaka huu.

Mchezaji wa tenesi raia wa Uswis, Roger Federer
Mchezaji wa tenesi raia wa Uswis, Roger Federer Reuters/Adrees Latif
Matangazo ya kibiashara

Federer mwenye umri wa miaka 35 hivi sasa amekuwa nje ya uwanja toka mwishoni mwa mwezi Julai, ambao mechi yake ya mwisho kucheza ilikuwa ni katika nusu fainali ya mashindano ya Wimbledon dhidi ya Milos Raonic.

Bingwa huyu mara 17 wa mataji ya Grand Slams, alifanyiwa upasuaji mwezi February mwaka huu kutokana na matatizo ya mgongo ambapo alishindwa kushiriki hata kwenye mashindano ya French Open.

β€œNafanya jitihada kujiandaa kwaajili ya mashindano ya Australian Open, naendelea vizuri kwakweli.” Alisema Federer.

β€œSikuwa nimewaza kuwa naweza kuwa na mwaka kama huu. Nimejifunza mengi mwaka huu,” aliongeza Federer ambaye alishindwa pia kushiriki michezo ya Olimpiki ya mwaka huu iliyofanyika Rio, Brazil na pia atashindwa kujaribu kutwaa taji lake la 6 la michuano ya US Opne inayoanza Agosti 29 mwaka huu.

Federer amesema haya wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari mjini New York, Marekani wakati akizundua mashindano mapya yanayofahamika kama β€˜Laver Cup’ ikifanana kabisa na michuano ya Ryder-Cup, yaliyopoewa jina la mkongwe wa Australia Rod Laver na yanatarajiwa kuanza mwezi September mwakani na kuchezwa duniani kote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.