Pata taarifa kuu
PARALYMPIC-RIO

Wanamichezo wa Urusi wenye ulemavu wazuiliwa kushiriki michezo ya Olimpiki mwezi ujao

Nchi ya Urusi haitashiriki kwenye michezo ya mwezi ujao ya watu wenye ulemavu, inayofanyika nchini Brazil, baada ya kushindwa kwenye rufaa yake waliyokata kupinga uamuzi wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu. 

Nembo ya kamati ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu, Urusi.
Nembo ya kamati ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu, Urusi. IPC
Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya kimataifa ya michezo (Cas) imeunga mkono uamuzi wa kamati ya kimataifa ya Olimpiki kwa watu wenye ulemavu (IPC) wa kuwafungia wanamichezo wote wa Urusi waliokuwa washiriki mwezi ujao.

Kamati ya IPC ilichukua uamuzi huo ikizingatia ripoti iliyochapishwa na taasisi ya MacLaren, ambayo ilianisha kwa kina namna Serikali ilivyoshiriki kuwasaidia wanamichezo wake kukwepa vipimo vya kubaini ikiwa walitumia dawa za kusisimua misuli au la.

Mchezaji wa Urusi mwenye ulemavu kwenye mchezo wa barafu, ambao hawataruhusiwa kushiriki.
Mchezaji wa Urusi mwenye ulemavu kwenye mchezo wa barafu, ambao hawataruhusiwa kushiriki. RPC

Michezo Paralympic inatarajiwa kuanza kutimua vumbi mjini Rio, kuanzia September 7.

Kwa mujibu wa hukumu ya Cas, imesema kuwa, uamuzi uliochukuliwa na IPC ulikuwa muafaka kwa kuzingatia mazingira na kwamba itachapisha taarifa yake yote kueleza ni kwanini imefikia kwenye uamuzi wa kuunga mkono adhabu ya IPC.

Kwenye maelezo yake ya awali, Cas inasema kuwa kamati ya Olimpiki ya Urusi kwa watu wenye ulemavu, haikuwasilisha ushahidi wowote muhimu kuonesha ukinzani wao na maamuzi ya IPC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.