Pata taarifa kuu
RIADHA

Farah agusia kustaafu baada ya mashindano ya dunia ya London mwakani

Bingwa mara nne wa medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki, Muingereza Mo Farah, amesema anapanga kustaafu mchezo huo mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya dunia ya mwaka ujao jijini London, lakini hakuficha nia yake ya kutaka kukimbia Marathon kwenye michezo ya Olimpiki ya mwaka 2020, mjini Tokyo, Japan. 

Mwanariadha wa Uingereza, Mo Farah akiwa amevaa medali zake mbili za dhahabu alizoshinda kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil.
Mwanariadha wa Uingereza, Mo Farah akiwa amevaa medali zake mbili za dhahabu alizoshinda kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil. REUTERS/Dylan Martinez
Matangazo ya kibiashara

Farah mwenye umri wa miaka 33, amekuwa mwanariadha wa Uingereza aliyepata mafanikio zaidi kwenye ugawa wa michezo ya Olimpiki, ambapo Jumamosi ya Agosti 20 alishinda medali ya dhahabu kwenye mbio za mita 5000.

Hii ilikuwa medali yake ya pili mjini Rio, Brazil, baada ya kushinda medali nyingine ya dhahabu katika mbio za mita 10000.

"Mwaka 2017, ningependa kustaafu kukimbia kwenye uwanja na tuone vile ambavyo naweza kufanya kwenye Marathoni," alisema Mo Farah.

Farah ambaye alimaliza kwenye nafasi ya 8 kwenye mbio za Olimpiki London mwaka 2012, atakuwa na umri wa miaka 37 wakati michezo ya Tokyo itakapofanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.