Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016

Toth aishindia Slovakia medali ya dhahabu katika mashindano ya kutembea

Matej Toth kutoka Slovakia ndio bingwa wa mashindano ya kutembea ya Kilomita 50 kwa upande wa wanaume katika Michezo ya Olimpiki nchini Brazil.

Matej Toth  bingwa wa Olimpiki michezo ya Olimpiki 2016
Matej Toth bingwa wa Olimpiki michezo ya Olimpiki 2016 Olympic 2016
Matangazo ya kibiashara

Toth ambaye pia ni bingwa wa dunia alimaliza wa kwanza kwa muda wa saa 3 dakika 40 na sekunde 58 na kuipa nchi yake medali ya dhahabu siku ya Ijumaa.

Jared Tallent raia wa Australia ambaye alikuwa bingwa mtetezi wa Michezo hii ya Olimpiki, alishindwa kutetea taji lake baada ya Toth kumpita na akamaliza wa pili.

Medali ya shaba ilimwendea Mjapan Hirooki Arai.

Mfaransa Yohann Diniz ambaye alionekana akiongoza kwa Kilomita za kwanza 30, alilemewa na hata wakati mmoja kuonekana kukata tamaa.

Kutokana na joto jingi katika mji wa Rio de Janeiro, watembeaji wengi walijiondoa katika mashindano hayo huku wengine pia wakiondolewa kwa kwenda kinyume na kanuni.

Watembeaji wakipambana katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 nchini Brazil
Watembeaji wakipambana katika Michezo ya Olimpiki ya mwaka 2016 nchini Brazil olympic.org

Katika mashindano ya Kilomita 20 pia kwa wanaume, Wang Zhen kutoka China alinyakua medali ya dhahabu baada ya kumaliza kwa muda wa saa 1 dakika 19 na sekunde 14.

Mwenzake pia kutoka China Cai Zelin pia kutoka China alimaliza wa pili kwa muda wa saa 1 dakika 19 na sekunde 26, huku nafasi ya tatu ikimwendea Dane Bird-Smith wa Australia aliyemaliza kwa muda wa saa 1 dakika 19 na sekunde 37.

Kanuni ya mchezo huu ni kuwa hakuna kukimbia katika riadha na ni lazima kwa miguu kuonekana ikikanyaga ardhi wakati wote wa mashindano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.