Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-SOKA

Nigeria kumenyana na Ujerumani nusu fainali michezo ya Olimpiki

Michuano ya nusu fainali kuwania medali ya ghahabu katika Michezo ya Olimpiki inachezwa siku ya Jumatano nchini Brazil.

Matangazo ya kibiashara

Mchuano wa kwanza utakuwa ni kati ya wenyeji Brazil watakomenyana na Honduras, na baadaye Nigeria dhidi ya Ujerumani.

Nigeria ambayo imekuwa ikionesha mchezo mzuri hadi kufikia hatua hii, ilifuzu katika hatua ya nusu fainali baada ya kuishinda Denmark mabao 2 kwa 0 Jumamosi iliyopita.

Mashabiki wa soka barani Afrika na wachambuzi wa soka wanasema, mechi dhidi ya Nigeria na Ujerumani itakuwa ngumu lakini inaleta matumaini ya Super Eagles kufika fainali na hata kushinda taji hili kama ilivyokuwa mwaka 1996.

Kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria inayoshiriki katika Michezo ya Olimpiki
Kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria inayoshiriki katika Michezo ya Olimpiki standard.co.uk

Ujerumani nayo ilifuzu baada ya kuifunga Ureno mbao 4 kwa 0 katika mchezo wa robo fainali, Honduras ikaishinda Korea Kuisni bao 1 kwa 0 na wenyeji Brazil wakawalemea Colombia mabao 2 kwa 0.

Fainali itachezwa mwishoni mwa wiki hii.

Kwa upande wa wanawake, Sweden itamenyana na Ujerumani siku ya Ijumaa kutafuta medali ya dhahabu katika mchuano wa fainali.

Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya  Ujerumani wakisherehekea baada ya kufuzu katika fainali ya Michezo ya Olimpiki mwaka 2016
Wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake ya Ujerumani wakisherehekea baada ya kufuzu katika fainali ya Michezo ya Olimpiki mwaka 2016 olympic.org

Sweden ilifuzu baada ya kuwashinda wenyeji Brazil kwa mabao 4 kwa 3 kupitia mikwaju ya penalti huku, Ujerumai ikaishinda Canada mabao 2 kwa 0.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.