Pata taarifa kuu
FFF-BENZEMA-SOKA

FFF: Karim Benzema kutoshiriki Euro 2016

Karim Benzema hatoshiriki kwa timu ya taifa ya Ufaransa katika michuano ya Kombe la mataifa ya Ulaya (Euro 2016).

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema, wakati wa mazoezi kabla ya mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Armenia Oktoba 8, 2015 katika uwanja wa Allianz Riviera, jijini Nice.
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema, wakati wa mazoezi kabla ya mechi ya kirafiki kati ya Ufaransa na Armenia Oktoba 8, 2015 katika uwanja wa Allianz Riviera, jijini Nice. MATTHIEU ALEXANDRE/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa ametangaza Jumatano hii, Aprili 13, kwenye Twitter, kwamba hatochaguliwa kushiriki michuano ya Ulaya itakayopigwa nchini Ufaransa kwa kipindi cha mwezi mmoja, kuanzia Juni 10 hadi Julai 10.

Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF), Noël

Le Graët, na kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, wameamua kumtenga mchezaji huyo, tangazo la FFF limebainisha.

"Hata kama imetokea, Bleu siku moja ... Blue milele"

Shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) limechukua uamuzi wake juu ya mustakabali wa mchezaji wa Real Madrid katika timu ya taifa ya Ufaransa, anayebanwa, kwa sababu ya matatizo yake ya kisheria. FFF ilitangaza "Benzegol" "hatoshirikishwa" baada ya kufanyiwa uchunguzi mwezi Novemba katika kesi ya madai ya mkanda wa usaliti kuhusu ngono dhidi ya mchezaji mwenzake wa timu ya taifa ya Ufaransa (Le Bleu) Mathieu Valbuena. Uamuzi wa Mahakama wa kumkataza kukutana na kiungo wa kati wa klabu ya Lyon, hata hivyo ulifutwa mwezi uliopita, na kupelekea shirikisho la Soka la Ufaransa (FFF) kutafakari.

Jumanne usiku, baada ya Real Madrid kufuzu nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa, Karim Benzema alisema kuwa alisubiri kwa "uaminifu" uamuzi wa FFF. Karim Benzema alirusha hewani kwenye ukurasa wake wa Facebook ujumbe uliyojaa kashfa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.