Pata taarifa kuu
AFCON 2017-GABON-SOKA

Fainali ya mataifa bingwa 2017

Mataifa 52 ya Afrika kwa mara nyingine, yanashiriki katika michuano muhimu ya soka kufuzu katika fainali ya mataifa bingwa itakayochezwa mwaka ujao wa 2017 nchini Gabon.

Timu ya taifa ya Côte d'Ivoire katika michuano ya CHAN 2016.
Timu ya taifa ya Côte d'Ivoire katika michuano ya CHAN 2016. Courtesy of cafonline
Matangazo ya kibiashara

Mataifa 16, wakiwemo wenyeji Gabon ambao tayari wamefuzu kwa sababu ni wenyeji watashiriki katika michuano hiyo.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya, nchi itakayokuwa wenyeji pia inashiriki katika michuano ya kufuzu lakini michuano hiyo itahesabiwa kama ya kirafiki, kuisadia kujiandaa kwa michuano hii.

Wenyeji Gabon wamejumuishwa pamoja na Sudan, Côte d’Ivoire na Sierra Leone.

Michuano iliyopita, Gabon ilitoka sare ya kutofungana na Côte d’Ivoire mwezi Juni mwaka 2015 na baadaye ikawashinda Sudan mabao 4 kwa 0 mwezi Septemba pia mwaka uliopita.

Wiki hii, Gabon umeratibiwa kucheza na Sierra Leon.

Mshindi wa kundi hili ndiye atakayefuzu katika fainali ya AFCON kwa sababu ina timu tatu ambazo alama zake zinahesabiwa.

Mbali na hili, kuna makundi 13 na mshindi katika kila kundi atafuzu lakini timu 2 zitakazokuwa zimemaliza katika nafasi ya pili kwa matokeo mazuri pia yatafuzu na kuungana pia na Gabon.

Hadi sasa mabao 126 yamefungwa tangu kuanza kuchezw akwa michuano hii ya kufuzu mwezi Juni mwaka uliopita.

Wachezaji wanaongoza katika safu ya ufungaji ni pamoja na El Arbi Hillel Soudani kutoka Algeria, Ferebory Dore kutoka Congo Brazavile na Basem Morsy wa Misri wamefunga mabao 4 kila mmoja.

Eritrea na Somalia ndio mataifa pekee ambayo hayasikriki katika michuano hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.