Pata taarifa kuu
CHAN 2016-RWANDA

Chan 2016: Côte d’Ivoire yafuzu robo fainali

Timu ya Côte d'Ivoire imetetea nafasi yake katika robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika, Jumapili hii Januari 24 katika uwanja wa mpira wa Huye, ikiilambisha Gabon mabao 4-1.

Timu ya taifa ya Côte d'Ivoire katika michuano ya CHAN 2016.
Timu ya taifa ya Côte d'Ivoire katika michuano ya CHAN 2016. Courtesy of cafonline
Matangazo ya kibiashara

Morocco, ambaye imeifungwa mabao 4-1 Rwanda ambayo tayari imefuzu robo fainali, pamoja na Gabon ambazo zote ni kutoka kundi A, zimeaga michuano hii ya CHAN 2016. Morocco inachukua nafasi ya 3, nayo Gabon inachukua nafasi ya 4.

Morocco na Gabon,a mbazo zilifuzu robo fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika 2014, zimeshindwa kufikia hatua hii katika makala ya CHAN 2016 nchini Rwanda. Timu hizi mbili kutoka kundi A zimeaga mapema michuano hii. Gabon timejikuta, hadi dakika 90 za mchezo imeburuzwa na Côte d'Ivoire mabao 4-1.

Mapema katika kipindi cha kwanza, timu zote mbili zilishindwa kila mmoja kufika kwenye lango la mwengine. Mikwaju ilikua ikipigiwa kwa mbali. Kiungo wa Côte d'Ivoire Essis Aka Baudelaire ni wa kwanza kuliona lango al Gabon, baada ya majaribio kadhaa ya pande zote mbili. Bao hili la kwanza la Côte d'Ivoire lilifungwa katika dakika ya 20 kwenye mita 25.

Mpaka sasa Rwanda ndio inachukua nafasi ya kwanza katika kundi A, na Côte d'Ivoire inachukua nafasi ya pili katika kundi hili. Morocco inachukua nafasi ya 3, nayo Gabon inachukua nafasi ya 4.

Timu za kundi A jinsi zinavyoshindana

1. Rwanda pointi 6 - imefuzu
2. Côte d'Ivoire pointi 6 - imefuzu
3. Maroc pointi4 - imeaga michuano
4. Gabon pointi 1 - imeaga michuano

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.