Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-AFRIKA

Soka mchezaji bora barani Afrika

Mchezaji bora wa soka barani Afrika mwaka 2015, atafahamika siku ya Ahamisi mjini Lagos nchini Nigeria.

Katika mji wa Lagos ambako kunatazamiwa kufanyika uchaguzi wa mchezaji bora barani Afrika mwaka 2015.
Katika mji wa Lagos ambako kunatazamiwa kufanyika uchaguzi wa mchezaji bora barani Afrika mwaka 2015. PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji watatu wanaowania taji hilo ni pamoja na Andre Ayew kutoka Ghana anayechezea klabu ya Swansea City nchini Uingereza, Pierre-Emerick Aubameyang kutoka Gabon anayechezea Borussia Dortmund ya Ujerumani, na Yaya Touré raia wa Cote d'Ivoire anayechezea Manchester City nchini Uingereza.

Touré atakuwa mchezaji wa kwanza kushinda taji hili mara tano mfululizo ikiwa atashinda.

Kiungo mshambuliaji huyo wa Manchester City, alishinda taji hili mara ya kwanza mwaka 2011, 2012, 2013 na 2014.

Mchezaji mwingine ambaye ametia fora katika tuzo hizi ni Samuel Eto'o kutoka Cameroon ambaye siku hizi anacheza soka la kulipwa nchini Uturuki, alishinda mataji manne mwaka 2003, 2004, 2005 na 2010.

Kwa upande wa wachezaji wanaocheza soka barani Afrika, wanaowania tuzo hii ni pamoja na Baghdad Boundjah raia wa Algeria anayechezea Etoile du Sahel ya Tunisia, Mbwana Aly Samata kutoka Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kipa Robert Kidiaba kutoka DR Congo anayechezea TP Mazembe.

Makundi mengine ni :

Mchezaji bora wa kike

  • Gabrielle Onguéné, Cameroon
  • Gaelle Enganamouit, Cameroon
  • Ngozi Ebere, Nigeria
  • N'rehy Tia Ines, Cote d’Ivoire
  • Portia Boakye, Ghana

Mchezaji chipukizi wa mwaka

  • Adama Traoré, Mali
  • Kelechi Nwakali, Nigeria
  • Samuel Diarra, Mali
  • Victor Osimhen, Nigeria
  • Yaw Yeboah, Ghana

Mchezaji mwenye kipaji

  • Azubuike Okechukwu, Nigeria
  • Etebo Oghenekaro, Nigeria
  • Djigui Diarra, Mali
  • Mahmoud Abdelmonem ‘kahraba’, Egypt
  • Zinedine Ferhat, Algeria
  • Kocha wa mwaka
  • Baye Ba, Mali, U17
  • Emmanuel Amunike, Nigeria U17
  • Fawzi Benzarti, Etoile Sportive de Sahel
  • Hervé Renard, Cote d’ivore
  • Patrice Carteron, TP Mazembe

Refarii wa mwaka

  • Alioum Neant, Cameroon
  • Bakary Papa GASSAMA, Gambia
  • Eric Arnaud OTOGO CASTANE, Gabon
  • Ghead Zaglol GRISHA, Egypt
  • Janny SIKAZWE, Zambia

Tuzo la heshima

  • Charles Kumi Gyamfi, Ghana
  • Samuel Mbappé Léppé, Cameroon

Timu ya mwaka

  • Cote d’Ivoire
  • Ghana
  • Mali U17
  • Nigeria U17
  • Nigeria  U-23

Timu ya taifa ya wanawake

  • Ghana
  • Cameroon
  • South Africa
  • Zimbabwe

Klabu ya mwaka

  • USM Algers , Algeria
  • TP Mazembe, DR Congo
  • Orlando Pirates, South Africa
  • Etoile Sportive du Sahel, Tunisia

Historia ya tuzo hizi:

Tuzo hii hutolewa kila mwaka huu.
Mchezaji bora Mwafrika anayecheza nyumbani na nje ya bara la Afrika hutuzwa.
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limekuwa likishughulikia tuzo hizi tangu mwaka 1992.

Gazeti la michezo kutoka Ufaransa lilikuwa linatoa tuzo hizi tangu mwaka 1970 hadi 1994.

Wachezaji wa kwanza kabisa kupokea tuzo hii walikuwa ni pamoja na Abedi Pele kutoka Ghana mwaka 1992.

  • Rashidi Yekini kutoka Nigeria mwaka 1993
  • Emmanuel Amuneke raia wa Nigeria mwaka 1994
  • George Weah kutoka Liberia mwaka 1995

Wengine

  • Nwankwo Kanu kutoka Nigeria mwaka 1996
  • Victor Ikpeba kutoka Nigeria mwaka 1997
  • Mustpha Hadji kutoka Morocco mwaka 1998
  • Nwankwo Kanu kutoka Nigeria mwaka 1999
  • Patrick Mbona kutoka Cameroon mwaka 2000
  • El Hadji Diouf kutoka Senegal mwaka 2001 na 2002
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.