Pata taarifa kuu
SOKA-LIGI KUU YA UINGEREZA

Liverpool yaangukia pua kwa kufungwa na Newcastle

Timu za Liverpool na Newcastle zimepimana nguvu Jumapili hii katika uwanja wa mpira wa St james Park katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza inayoendelea.

Demba Ba, raia wa Senegali, ambaye anaichezea Newcastle, akijikuta katika wafu bada ya kuingiza bao la pili.
Demba Ba, raia wa Senegali, ambaye anaichezea Newcastle, akijikuta katika wafu bada ya kuingiza bao la pili. REUTERS/Nigel Roddis
Matangazo ya kibiashara

Newcastle ikichezea nyumbani imetikisa nyavu za Liverpool mara mbili, na kufanikiwa kupata ushindi wa mabao mawili kwa nunge hadi kipenga cha mwisho.

Bao la kwanza la Newcastle limefungwa na Martin Skrtel wa Liverpool, ambaye alijikuta amejifunga katika harakati ya kuoko mpira uliopigwa na mchezaji nyota wa Newcastle, Georgino Winaldum. Bao hilo liliingizwa katika dakika ya 69 ya mchezo.

Katika dakika ya 93 yaani muda wa nyongeza Newcastle walikuja juu na kuingiza bao la pili, bao lililowekwa kimyani na Wina-Naldum.

Kwa sasa Newcastle wanachukua nafasi ya 18 wakiwa na alama 18 mbele ya Sunderland na Aston Villa. Timu hizi mbili zinachukua nafasi ya mwisho katika msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Na leo Jumatatu klabu za Everton na Crystal Palace zitamenyana, ambapo Everton watakua nyumbani wakiwakaribisha Crystal Palace.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.