Pata taarifa kuu
KENYA-RIADHA

Kenya: Jackson Tuwei rais wa mpito wa Shirikisho la Riadha

Shirikisho la Riadha nchini Kenya (AK), Jumanne hii, limemteua mkuu wa zamani wa jeshi, Jackson Tuwei, kuwa rais wa mpito wa Shirikisho la Riadha nchini humo, akichukua nafasi ya Isaiah Kiplagat, aliyesimamishwa na Shiriisho la kimataifa la Riadha (IAAF) kwa tuhuma za rushwa.

Wanariadha wa Kenya wakifanya mazoezi nje ya makao makuu ya Shirikisho la lao, Novemba 23, 2015 jijini Nairobi.
Wanariadha wa Kenya wakifanya mazoezi nje ya makao makuu ya Shirikisho la lao, Novemba 23, 2015 jijini Nairobi. AFP/AFP/Archive
Matangazo ya kibiashara

Uteuzi wa Tuwei umetangazwa baada ya mkutano wa kamati tendaji ya Shirikisho la Riadha nchini Kenya, ambalo limebainisha kusimamishwa kwa maafisa wake watatu waliolengwa na uchunguzi wa IAAF na kuahadi kushirikiana na mamlaka.

"Baada ya kusimamishwa kwa rais wa AK na tume ya maadili ya IAAF, kamati tendaji imeamua kumteua Luteni Jenerali Jackson Kiprono Tuwei kwa uamzi wa haraka", taarifa kutoka Shirikisho la kitaifa la Riadha imesema.

Rais wa zamani Kiplagat, Makamu wake Rais, Daudi Okeyo, na mweka hazina wa zamani, Joseph Kinyua, walisimamishwa kwenye nafasi zao kutokana na uchunguzi wa tuhuma dhidi yao kwa "mchakato unaoendelea wa kuchunguza wanariadha wanaotumia dawa za kusisimua misuli nchini Kenya na matumizi mabaya ya fedha zilopokelewa na Shirikisho la Riadha la Kenya (AK) kutoka kampuni ya Nike. "

Okeyo, ambaye alikua akishiriki vikao vya bodi ya IAAF ambapo alikua akishikilia nafasi ya Mkurugenzi msimamizi wa mashindano, atajikuta nafasi yake imekabidhiwa mjumbe mwengine wa kamati tendaji.

Mwendesha mashitaka wa zamani wa Kenya, Sharad Rao, ameteuliwa na Shirikisho la kimataifa la Riadha kupitia upya mashtaka dhidi ya maafisa hao watatu waliosimamishwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.