Pata taarifa kuu
RIADHA-MCHEZO

Viongozi wapya wa mchezo wa riadha duniani kuchaguliwa

Mkutano Mkuu wa Shirikisho la riadha duniani IAAF unafanyika siku ya Jumanne na Jumatano wiki hii jijini Beijing nchini China.

raia wa Kenya katika mbio za Boston marathon, Aprili 21 mwaka 2014.
raia wa Kenya katika mbio za Boston marathon, Aprili 21 mwaka 2014. AFP PHOTO / Timothy A. CLARY
Matangazo ya kibiashara

Ajenda kuu ya mkutano huo ni kuwachagua viongozi wapya kuongoza mchezo huo duniani na kuzungumzia maswala yanayoukumba mchezo huo.

Wadhifa wa urais unagombewa na watu wawili Sebastian Coe raia wa Uingereza na Sergei Bubka raia wa Ukraine kuchukua nafasi ya Lamine Diack raia wa Senegal ambaye anastaafu baada kuongoza Shirikisho hilo kwa miaka 16 sasa tangu mwaka 1999.

Kura hiyo itapigwa siku ya Jumatano na mshindi kati ya Bubka ambaye zamani alikuwa anashiriki mchezo wa kuruka wa Pole Vault na mwanariadha wa zamani wa mbio fupi Coe atakuwa rais mpya wa IAAF.

Mbali na wadhifa wa urais, wajumbe pia watawachagua Makamu wanne wa urais na wagombea saba wanawania nyadhifa hizo.

Miongoni mwao ni rais wa Shirikisho la riadha nchini Kenya Isaih Kiplagat na Hamas Kalkaba Malboum ambaye anaongoza riadha nchini Cameroon ambao wanaliwakilisha bara la Afrika.

Uchaguzi huu unakuja wakati huu Shirikisho hilo likikabiliwa na madai kuwa wanariadha wengi wanaoshinda mashindano mbalimbali ya dunia wameendelea kutumia dawa za kusisimua misuli.

Majumaa kadhaa yaliyopita, Gazeti la Uingereza la Sunday Times na runinga ya Ujerumani ya ARD vilitoa ripoti kuwa tabia ya wanariadha kutumia dawa hizo imeongezeka sana katika siku za hivi karibuni.

Pamoja na hayo, mkutano huu utamalizika siku moja kabla ya kuanza kwa mashindano ya duani ya raidha yatakayofanyika jijini Beijing kati ya tarehe 22 hadi tarehe 30 mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.