Pata taarifa kuu
CECAFA-MICHUANO 2014

CECAFA yafutilia mbali michuano ya mwaka 2014

Baraza la soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA limetangaza kuwa, michuano ya mwaka huu baina ya timu za taifa imefutiliwa mbali.

Wakishiriki michuano ya Kombe la CECAFA Cup, wachezaji kumi na wawili wa  Eritrea walitoweka mjini Nairobi.
Wakishiriki michuano ya Kombe la CECAFA Cup, wachezaji kumi na wawili wa Eritrea walitoweka mjini Nairobi. AFP
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa CECAFA Nicholas Musonye amesema kuwa michuano ya mwaka huu imefutuliwa mbali baada ya kukosekana na mwenyeji wa michuano hiyo kuchukua nafasi ya Ethiopia iliyojiondoa katika dakika za lala salama.

Uaumuzi huo ulifikiwa mwishoni mwa juma lililopita baada ya kikao cha viongozi wa soka kutoka eneo la Afrika Mashariki na Kati uliofanyika jijini Nairobi nchini Kenya.

Musonye ameongeza kuwa, mipango itafanyika ili kubadilisha mfumo wa michuano hiyo ili kuvutia zaidi katika siku zijazo.

Rwanda itakuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwaka ujao wa 2015. Mabingwa watetezi ni Kenya walionyakua taji hilo mwaka uliopita wakati michuano hiyo ilipoandaliwa jijini Nairobi.

Mbali na hilo, viongozi wa CECAFA wameamua kwa kauli moja kuwa watamuunga mkono rais wa sasa wa FIFA Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 78 kuwania tena urais wa Shirikisho hilo kwa muhula wa Tano mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.