Pata taarifa kuu
LIGI YA MABINGWA / ULAYA

Ligi ya Mabingwa: Monaco yapata ushindi wa kifahari

Katika mchuano ambao ulivutia masahbiki na watazamaji, AS Monaco ikichezea ugenini imepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bayer Leverkusen kupitia mchezaji wake Ocampos.  

Ocampos akiifungia klabu yake ya Monaco dhidi ya Bayer Luverkusen.
Ocampos akiifungia klabu yake ya Monaco dhidi ya Bayer Luverkusen. REUTERS/Ina Fassbender
Matangazo ya kibiashara

Matokeo haya hayajaipa Monaco ushindi wa kufuzu mzunguko wa nane wa michuano ya klabu bingwa. Monaco inahitaji angalau kwenda sare ya kutofungana dhidi ya Zenit St Petersburg.

Ushindi huu wa Monaco dhidi ya Bayer Leverkusen ni wa pili, ambao utapelekea klabu hiyo kuimarisha kikosi chake ili waweze kufuzu mzungulko wa nane wa lidi ya mabingwa.

Saa moja kabla ya mchuano huo kati ya Monaco na Bayer Leverkusen kuanza, kalabu ya Zenith Saint-Pétersbourg iliimenyana na Benfica. Hadi kipenga cha mwisho Benfica iliburuzwa na Zenith Saint-Pétersbourg kwa bao 1-0.

Katika kipindi cha kwanza Bayer Leverkusen ilitawala mpira, licha ya kuwa Monaco iliendelea kudhibiti hali hiyo.

Monaco ilipachika bao hilo katika dakika ya 72 kupitia mchezaji wake Ocampos, baada ya kumrudilia Carrasco.

Kwa sasa Monaco inaongoza kwa alam 8, ikichukua nafasi ya pili katika kundi C. Monaco inajianda kumenyana na Zenith St Petersbourg Decemba 9.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.