Pata taarifa kuu
Soka Barani Afrika

Timu ya taifa ya Ghana yamtafuta kocha mpya

Nchini Ghana, Mholanzi Patrick Kluivert ni miongoni mwa makocha watano wanaopendekezwa kuchukua nafasi ya mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Black Stars ya Ghana.

Mashabiki wa timu tya taifa ya Ghana Black Stars.
Mashabiki wa timu tya taifa ya Ghana Black Stars. REUTERS/Brian Snyder
Matangazo ya kibiashara

Black Stars imekuwa haina kocha tangu mwezi uliopita baada ya kufutwa kazi kwa Kwesi Appiah.

Makocha wengine waliomba kazi ni pamoja na aliyekuwa kocha wa Chelsea Avram Grant,Kiungo wa kati wa zamani wa Italia Marco Tardelli, mswisi Michel Pont na mhispania Juan Ignacio Jimenez.

Kwa sasa, Maxwell Konadu ndiye Kaimu wa timu hiyo ya Ghana, Black Stars, ambayo inatafuta nafasi ya kucheza katika fainali ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Morroco.

Mwishoni mwa juma hili, Ghana itamenyana na Guinea mjini Casablanca nchini Morroco.

Nchini Mauritania, Mfaransa Corentin Martins ameteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya mchezo wa soka kuchukua nafasi ya Patrice Neveu, baada ya kushindwa kuingoza timu yake kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao.
Na nchini Zambia, Nico Labohm raia wa Uholanzi ameteuliwa kuwa naibu kocha wa Kocha mkuu Honour Janza.

Labohm atasaidiana na Janza kuisaidia Chipolopolo kutafuta nafasi ya kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka ujao nchini Morroco.

Zambia itakuwa ugenini jijini Niamey mwishoni mwa juma hili kumenyana na Niger, katika mchuano wa kwanza kutafuta ushindi wa kwanza katika kundi moja na Cape Verde na Msumbiji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.