Pata taarifa kuu
UINGEREZA-Michezo-Soka

Arsenal yatamba mwaka huu katika ngao ya Jumuiya

Klabu ya Arsenal ya Arsene Wenger imepata ushindi jana jumapili kwenye uwanja wa Wembley kwa kuifunga Manchester City mabao 3-0, baada ya Machester City kuonekana kushindwa mchezo

wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi wao dhidi ya Manchester City kwenye uwanja wa Wembley, Agosti 10 mwaka 2014.
wachezaji wa Arsenal wakifurahia ushindi wao dhidi ya Manchester City kwenye uwanja wa Wembley, Agosti 10 mwaka 2014. REUTERS/Andrew Winning
Matangazo ya kibiashara

Miezi mitatu, baada ya kushinda katika fainali ya michuano ya kombe la FA, Arsenal haikusubiri miezi tisa ili iandikishe upya rekodi yake.

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger akibaini kwamba matumani ya kuifunga Manchester City walikua nayo kabla hata ya mchezo kuanza.
Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger akibaini kwamba matumani ya kuifunga Manchester City walikua nayo kabla hata ya mchezo kuanza. REUTERS/Stefan Wermuth

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amekua na matumaini ya kushinda baada ya wachezaji wake kuingia uwanjani. Kwa muda wa dakika 90 za mchezo Arsenal imeonyesha ujuzi wake, baada ya kusajili wachezaji wenye uzowefu.

Mathieu Debuchy, Calum Chambers na Alexis Sanchez, ambao wote walisajiliwa msimu huu kwa kitita cha Uro milioni 80, walionekana wakitawala mpira. Wachezaji hao wamekuja kuipa nguvu klabu hiyo ambayo ilitwaa kombe la FA.

Baada ya dakika chache za mchezo huo kuanza, ambao ulitawaliwa kwa sehemu na Arsenal, santi Cazorla iliafanikiwa kuingiza bao la kwanza katika dakika ya 22, baadaye Aaron Ramsey akaingiza bao la pili katika dakika ya 42 kwa pasi nzuri aliyopewa na Sanogo.

Kipindi cha kwanza cha mchezo kilimalizika Arsenal ikiongoza mabao 2 kwa nunge.

Katika dakika ya 61, Arsenal ilikuja juu na kuingiza bao la tatu, ambalo liliingizwa na Olivier Giroud kwa mkwaju uliyopigwa kwa umbali wa mita 20. Bao hilo la tatu lilipelekea wachezaji wa Manchester city kukata tamaa

Wachezaji wa kati wa Manuel Pellegrini, kama vile Nasri, Touré - Fernando pamoja na Navas hawakua dafu mbele ya kikosi cha Arsenal, hata baada ya kuingia kwa David Silva.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.