Michuano ya kombe la dunia yaingia robo fainali
Michuano ya kombe la dunia inaendelea nchini Brazil, ambapo timu inne ziliyotinga robo fainali, zinajiandaa kupambana. Timu ya taifa ya Brazil inajianda kumenyana leo ijumaa na Colombia kwenye uwanja wa Fortaleza, huku Ujerumani na Ufaransa zikijiandaa kupambana kwenye uwanja wa Rio.
Imechapishwa:
Brazil ambayo inachezea nyumbani kwa macho ya mashabiki wengi, huku Ujerumani ikiwa inavuja kwenye safu ya ushambuliaji watalazimika kuongeza nguvu katika michuano hii dhidi ya wapinzani wao.
Katika mzunguko wa nane, Brazil na Ujerumani zililazimishwa kupitia kwenye kipindi cha muda wa dakika 30 za nyongeza. Vile vile Brazil ilinusurika kupitia mikwaju ya penalti (baada ya kutoka sare ya kufungana na Chili bao 1-1). katika mikwaju ya penalti, Brazil iliingiza wavuni mabao 3, huku Chili ikiingiza mabao 2.
Hayo yakijiri, Argentina-Ubelgiji na Uholanzi-Costa Rica zinajiandaa kumenyana jumamosi hii.
Rais wa Ufaransa François Hollande anaandaa ijumaa hii jioni hafla ya kirafiki kati ya Ufaransa na Ujerumani kwa niaba ya mchuano huu kati ya mataifa haya mawili.