Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Rais Rousseff atetea utayari wa nchi yake kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la Dunia 2014

Rais wa Brazil, Dilma Rousseff ametetea uamuzi wa nchi yake kuwa mwenyeji wa michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 na kwamba licha ya kasoro zinazoelezwa bado taifa lake liko tayari kuwa mwenyeji wa fainali hizi.

Rais wa Brazil, Dilma Rousseff
Rais wa Brazil, Dilma Rousseff Reuters
Matangazo ya kibiashara

Fainali hizi ambazo zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi juma lijalo mjini Sao Paulo, wachambuzi wa mambo na hasa wale wa soka wamekuwa wakikosoa vikali maandalizi ya fainali hizi nchini Brazil.

Akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari, rais Rousseff amesema kuwa fainali za mwaka huu zitakuwa za aina yake na taifa hilo litaweka historia licha ya ukosolewaji mkubwa.

Rais wa Brazil, Dilma Rousseff akiwa na rais wa shirikisho la mpira duniani fifa, Sepp Joseph Blatter
Rais wa Brazil, Dilma Rousseff akiwa na rais wa shirikisho la mpira duniani fifa, Sepp Joseph Blatter REUTERS/Thomas Hodel

Rais Rousseff anasema kuwa katika kila nchi ambako fainali hizi zimefanyika, zote zilikuwa zinakabiliwa na hali ngumu ya maandalizi na kwamba hakuna nchi ambayo iliweza kukamilisha ujenzi wa viwanja vyake kwa wakati na kwa asilimia mia moja.

Kauli ya rais Rousseff anaitoa wakati huu ambapo waandamanaji nchini humo wamepanga kufanya mgomo wa nchi nzima wakati wa fainali hizi, jambo ambalo rais amesema kuwa Serikali yake haitavumilia.

Waratibu wa maandamano ya kupinga fainali za kombe la dunia nchini Brazil, wamepanga kufanya maandamano mengine makubwa wakati fainali hizi zitakapoanza jambo ambalo rais Rousseff sasa ameagiza vikosi vyake kuwa makini na kuzuia maandamano yoyote yaliyopangwa kuharibu picha ya fainali za mwaka huu.

Kauli hii inatolewa wakati huu ambapo fainali hizi zinatarajiwa kuanza kutimua vumbi juma lijalo, huku karibu aslimia hamsini ya viwanja na miundo mbinu yake haijakamilika kwa asilimia mia, jambo ambalo huenda mechi nyingine zikachezwa kwenye viwanja ambavyo bado havijakamilika wala miundombinu yake.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.