Pata taarifa kuu
UEFA 2013/2014

Ronaldo avunja rekodi ya Messi ya kupachika mabao kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya

Hatimaye mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Christian Ronaldo amevunja rekodi ya kupachika mabao katika msimu mmoja wa michuano ya klabu bingwa barani Ulaya UEFA, akimpiku mpinzani wake, Lionel Messi wa FC Barcelona.

Sergio Ramos akifunga moja ya bao lililoipa ushindi timu yake
Sergio Ramos akifunga moja ya bao lililoipa ushindi timu yake fcbayern.de
Matangazo ya kibiashara

Rekodi hiyo ameivunja baada ya hapo jana kupachika mabao mawili kati ya manne ambayo timu yake ilifanikiwa kuchomoza na ushindi dhidi ya FC Barcelona, kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili ya klabu bingwa Ulaya.

Kufuatia mabao aliyofunga hapo jana, hii inamaanisha kuwa sasa Christiano Ronaldo amepachika nyavuni mabao 16 kati amechi 10 ambazo ameitumikia klabu yake kwenye msimu mmoja wa michuano hii.

PICHA ZAIDI

Ronaldo sasa anavunja rekodi iliyowahi kuwekwa kwa pamoja na mchezaji Lionel wa Barcelona kwenye msimu wa 2011-2012, Ruud van Nistelrooy aliyewahi kucheza Manchester United kwenye msimu wa mwaka 2002-2003 na ile iliyowekwa na Jose Altafini aliyewahi kucheza na AC Milan ya Italia kwenye msimu wa mwaka 1962 na 1963 ambao wote hawa walipachika mabao 14 kwenye msimu mmoja.

Mshambuliaji huyu wa zamani wa klabu ya Manchester United, sasa anakuwa amepachika mabao 67 katika historia yake ya mpira toka ameanza kushiriki kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Hapo jana mabao ya beki Sergio Ramos kwenye dakika ya 16 na 20 na yale ya Christian Ronaldo kwenye dakika ya 34 na 89 yalitosha kuipa timu yake ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Beyern Munich ambayo kwenye mchezo wa jana ilionekana kupoteana.

Kwenye mchezo uliopigwa juma moja lililopita mjini Madrid Uhispania, Madrid walifanikiwa kuchomoza na ushindi wa 1-0 dhidi ya Bayern.

Kwa ushindi wa hapo jana sasa unaifanya klabu ya Real Madrid kutinga katika hatua ya fainali ya michuano ya mwaka huu toka ilipofanya hivyo mwaka 2002 ambao ulikuwa ni mwaka wake wa mwisho kucheza fainali.

The ex-Manchester United forward has now scored 67 goals in his Champions League career, the same number as Messi and four shy of the record which is currently held by former Real and Schalke striker Raul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.