Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Katibu mkuu wa fifa, Jerome Valcke aridhishwa na ujenzi wa viwanja vya Brazil

Katibu mkuu mtendaji wa shirikisho la kabumbu duniani fifa, Jerome Valcke ameeleza kuridhishwa kwake na maandalizi ya uwanja wa Cuiaba ulioko katikati ya Brazil, licha ya uwanja huo kutokamilika kwa asilimia mia moja.

Waziri wa michezo wa Brazili, Aldo Rebelo (Kushoto), Mchezaji wa zamani wa Brazili Ronaldo Nazario (katikati) pamoja na Katibu mkuu wa fifa, Jerome Valcke wakiwa kwenye uwanja wa Cuiba
Waziri wa michezo wa Brazili, Aldo Rebelo (Kushoto), Mchezaji wa zamani wa Brazili Ronaldo Nazario (katikati) pamoja na Katibu mkuu wa fifa, Jerome Valcke wakiwa kwenye uwanja wa Cuiba fifa.com
Matangazo ya kibiashara

Valcke ametoa matamshi hayo saa chache baada ya kufanya ziara kwenye uwanja wa Cuiba moja kati ya viwanja ambavyo ujenzi wake ulikuwa bado haujakamilika na ilikuwa ni sehemu ya ziara yake kutembelea viwanja vitakavyotumika kwa michuano ya kombe la dunia mwaka huu.

Kiongozi huyo amesema kuwa licha ya kuwa uwanja huo haujakamilika kwa asilimia mia kutokana na kukoseakana kwa viti zaidi ya elfu 1 na 500, ameeleza matumaini yake kuwa uwanja huo utakamilika hata kabla ya kuanza kwa michuano ya mwaka huu.

PICHA ZAIDI

Kuchelewa kumalizika kwa uwanja wa Cuiaba kumetokana na mzozo wa kisheria uliokuwa mahakamani kati ya serikali na wakazi wa eneo uliko uwanja huo jambo ambalo limeufanya kuwa miongoni mwa viwanja ambavyo vimeshindwa kukamilika kwa wakati.

Valcke amewaambia waandishi wa Habari mjini Cuiaba kuwa hataki kuufananisha uwanja huo na viwanja vingine katika matayarisho yake, lakini akasisitiza kuwa anamatumaini kuwa mafundi watamaliza kabla ya wakati.

Juma hili katibu mkuu huyu alionesha hofu yake kwa baadhi ya viwanja kutokamilika kwa wakati vikwemo viwanja wa Sao Paulo ulioko kwenye mji wa Curitiba.

Uwanja huu ni moja ya kiwanja ambacho hakika kitakuwa cha mwisho kabisa kukamilishwa kwa ujenzi wake kutokana na mara kadhaa kusimama baada ya kutokea ajali ya kuanguka kwa jukwaa lake.

Kwa mujibu wa sheria za fifa kuhusu viwanja vitakavyochezewa kombe la dunia, ni lazima viwanja hivyo vikikamilika walau vichezewe kwa zaidi ya mara tatu ili kupima uwezo wake jambo ambalo Valcke anasema kwa uwanja wa Sao Paulo halitawezekana.

Uwanja wa Cuiaba unaelezwa na maofisa wa Brazil kuwa utakuwa tayari kabla ya tarehe 5 may siku chache kabla ufunguzi rasmi wa mashindano ya kombe la dunia.

Siku ya Alhamisi katibu mkuu Valcke ametembelea uwanja wa Aterro de Iracema, uwanja ambao utatumika kwa sherehe za mashabiki ambao watakuwa hawana uwezo wa kununua tiketi za kushuhudia michuano ya mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.