Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Katibu mkuu wa fifa kuzuru Brazil juma lijalo kwa ukaguzi zaidi wa viwanja

Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA wiki hii limesema kuwa katibu mkuu wake, Jerome Valcke anatarajiwa kusafiri kuelekea nchini Brazili juma lijalo kwa ukaguzi zaidi kwenye miji ya Sao Paulo, Curitiba, Cuiaba na Fortaleza ambako kuna viwanja ambako mechi zitachezwa.

Katibu mkuu wa shirikisho la kabumbu duniani, Jérôme Valcke.
Katibu mkuu wa shirikisho la kabumbu duniani, Jérôme Valcke. Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya katibu mkuu Valcke ni ya kila mwezi ambayo ilitangazwa kuwa hivyo na shirikisho hilo kwa kile ilichodai ni ufuatiliaji wa karibu kuhusu maandalizi ya viwanja ambavyo vitatumika kwaajili ya michuano ya kombe la dunia.

Wakati wa ziara yake, katibu mkuu Valcke ataambatana na waziri wa michezo wa Brazil Aldo Rebelo na kamati ya waandaaji wa michuano hiyo ikiongozwa na chama cha soka nchini humo.

Picha Zaidi

Ziara hii ni muhimu kwenye miji ambayo imetajwa kwa kile ambacho awali katibu mkuu huyu licha ya kuonesha matumaini yake ya viwanja vingi kukamilika kwa wakati lakini bado alisisitiza uangalizi wa karibu unahitajika.

Mfano mzuri ni uwanja wa mji wa Sao Paulo na Arena Corithians ambayo bado ujenzi wake haujakamilika kwa asilimia mia huku vikitegemewa kutumika wakati wa mechi za ufunguzi wa kombe la dunia kati ya Brazil na Croatia June 12.

Viwanja hivi vinatakiwa kukamilika kabla ya tarehe 20 May ambapo ndio muda wa mwisho uliotolewa na FIFA kwa nchi hiyo kuhakikisha viwanja vyote vinakuwa tayari kwaajili ya michuano ya mwaka huu.

Toka kuanza kwa ujenzi wa viwanja hivi kumekuwa na madhara kadhaa yaliyojitokea ambapo mwezi November mwaka jana na mwezi March mwaka huu watu wawili wameshapoteza maisha kwa kuangukiwa na jukwaa jambo ambalo linazusha hofu kuhusu usalama wa viwanja hivyo.

Utawala wa Brazil umekuwa ukikosolewa kutokana na viwanja vingi kutokuwa kwenye hali nzuri jambo ambalo wachambuzi wa mambo wameonya kuhusu uwezekano wa kutokea maafa iwapo viwanja vingine vitajaa kupita uwezo wake.

Kwenye ziara yake ya mwezi uliopita, katibu mkuu Valcke alikiri kuwepo kwa ucheleweshwaji wa ujenzi wa baadhi ya maeneo kama sehemu ya vyombo vya habari ambapo mpaka sasa maeneo mengi hayajakamilika jambo ambalo amesema ni changamoto kwa nchi nyingine ambazo zitapata nafasi ya kuandaa fainali hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.