Pata taarifa kuu
Michezo

Kiungo wa Klabu ya Arsenal Jack Wilshere kukaa nje ya uwanja kwa majuma sita

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal  Jack Wilshare atakaa nje ya uwanja kwa kipindi cha majuma sita baada ya kuumia wakati akiichezea timu ya taifa ya England dhidi ya Denmark juzi usiku katika mechi ya kirafiki. Hii itakuwa ni pigo kubwa sana kwa kalbu ya Arsenal kumkosa kiungo wake huyo kwa kipindi hicho. 

Kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere akiwa chini baada ya kuumia
Kiungo wa klabu ya Arsenal Jack Wilshere akiwa chini baada ya kuumia Actusports
Matangazo ya kibiashara

Jack Wilshere alianguka chini baada ya kugongana na Daniel Agger katika kipindi cha kwanza cha mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Wembley nchini Uingereza ambapo England ilishinda 1-0 bao ambalo lilipachikwa nyavuni na Danie Sturridge.

Kiungo huyo wa Arsenal atakosa mechi ya Raundi ya sita ya Kombe la FA, ambapo Arsenal itamenyana na Everton Jumapili, mechi ya marudiano na Bayern Munich Ligi ya Mabingwa Ulaya Hatua ya 16 Bora na mechi kadhaa za Ligi Kuu ya England zikiwemo dhidi ya Tottenham, Chelsea, Swansea City, Manchester City, Everton na West Ham.

Jack Wilshere anaweza kuwa tayari kurejea uwanjani katika mchezo na Hull City Aprili 19 na kisha kuanza kupambana na kurudi katika kiwango chake kuwania nafasi ya kuwemo kwenye kikosi cha England kitakachokwenda Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia katikati ya mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.