Pata taarifa kuu
USWISI-FIFA

Christiano Ronaldo apata tuzo la mchezaji bora wa soka duniani

Kama ilivyokuwa imetabiriwa na mashabiki wengi wa soka dunia, Mchezaji wa Kimataifa wa Ureno na anayesakata soka la kulipwa katika klabu ya Real Madrid ya Uhispania Cristiano Ronaldo ndiye mchezaji bora wa soka duniani mwaka 2013.

Matangazo ya kibiashara

Ronaldo alipata tuzo hilo katika Makao Makuu ya Shirikisho la soka duniani FIFA mjini Zurich nchini Uswizi jana Usiku na kuwashinda wachezaji wengine kama Lionel Messi aliyewahi kushinda taji hili kwa muda wa miaka minne mfululizo na Frank Ribery wa Bayern Munich ya Ujerumani.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 aliyefunga mabao 66 katika michuano 56 katika klabu yake na timu yake ya taifa alishinda kwa alama 1,365 , Messi akaibuka wa pili kwa alama i (1,205) na Ribery akamaliza wa tatu kwa alama (1,127),

Ronaldo anasema kuwa tuzo hili litamfafanya atie bidii zaidi msimu huu na ndoto yake ya kuwa mchezaji bora duniani imetimia.

Kura zilipigwa na Makocha 184 duniani, na Manahodha 184 pamoja na waandishi wa Habari 173 wa Michezo kutoka Duniani.

Kwa upande wa akina dada Kipa wa Timu ya taifa ya Ujerumani Nadine Angerer alitangazwa kuwa mchezaji bora.

Naye Jupp Hey -Ckes aliyekuwa Kocha wa Bayern Munich alitajwa kuwa kocha bora wa mwaka 2013.

Naye mchezaji wa Zamani wa Brazil Pele alipata tuzo la heshima kutoka kwa FIFA, huku Shirkisho la soka nchini Afganistan ndilo shirikisho bora la mwaka uliopita kutokana na juhudi zake za kuendeleza mchezo wa soka licha ya taifa hilo kukabililiwa na vita mara kwa mara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.