Pata taarifa kuu
SOKA

Carlo Ancelotti: Hatuna mpango wa kumsajili Radamel Falcao

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti amekanusha tuhuma kuwa klabu yake inapanga kumsajili mchezaji wa Monaco, Radamel Falcao. Ancelotti amesema ni dhahiri kuwa mshambuliaji huyo ana kiwango kizuri lakini haoni kama ni sahihi kuwamo katika kikosi chake kwa sasa.

francetvinfo.fr
Matangazo ya kibiashara

Kocha Ancelotti amesema kwa sasa wanafurahia kikosi walichonacho kwa kuwa wachezaji wake wamekuwa wakifanya vizuri.

Katika siku za hivi karibuni kumekuwa na tetesi kuwa Falcao ambaye kwa ni majeruhi ataondoka katika yake ya sasa licha ya kujinga nayo kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili kwa uhamisho wa kitita cha Euro milioni 60 akitokea Atletico Madrid.

Madrid wameshinda mechi zote tano zilizopita, wakifanikiwa kupata jumla ya magoli 24 katika msimu huu na hii leo wanajiandaa kukutana na Osasuna.

Mechi nyingine za La Liga zinazopigwa hii leo ni kati ya Rayo Vallecano na Granada, Barcelona na Villareal, wakati Malaga watakutana na Getafe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.