Pata taarifa kuu
SOKA-CECAFA

Harambee Stars ya Kenya yanyakua ubingwa wa CECAFA

Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars ndio mabingwa wa taji la CECAFA linalowaniwa kila mwaka baina ya mataifa ya Afrika Mashariki na kati baada ya kuifunga Sudan mabao 2 kwa 0 katika fainali iliyochezwa siku ya Alhamisi katika uwanja wa Nyayo jijini Nairobi.

Matangazo ya kibiashara

Nahodha wa Harambee Stars Allan Wanga ndiye aliyeifungia timu yake mabao yote mawili katika fainali iliyochezwa siku ambayo Kenya ilikuwa inaadhimsiha miaka 50 ya uhuru wake.

Ushindi wa Kenya ni wa sita katika historia ya michuano hiyo ya CECAFA na mara ya mwisho ilinyakua taji hilo mwaka 2002 walipowafunga Tanzania walioKuwa wenyeji wa michuno hiyo mabao 3 kwa 2 katika fainali iliyochewa mjini Mwanza.

Kocha wa Kenya Adel Amrouche amesema kuwa mshikamano na bidiI ya wachezaji wake ndio ilikuwa sababau ya wao kunyakua taji hili baada ya Kenya kukosa kufanya hivyo mwaka uliopita walipofungwa na Uganda mabao 2 kwa 1 jijini Kampala.

Fainali ya michuano hii ilicheleweshwa kwa saa moja baada ya wachezaji wa Sudan kuzuiliwa kuondoka katika hoteli waliyokuwa wanaishi kutokana na kutoilipia na kusababisha serikali ya Kenya kuiongilia kati kuwanusuri wachezaji hao.

Kabla ya mchuano wa fainali Zambia waliokuwa wamealikwa katika michuano hiyo waliishinda Tanzania bara mabao 5 kwa 6 kupitia mikwaju ya penalti baada ya timu zote mbili kupata sare ya mabo 1 kwa 1 katika muda wa kawaida.

Michuano ya CECAFA iliandaliwa nchini Kenya kwa kipindi cha wiki mbili zilipita na kuchezwa katika miji mbalimbali kwa mara ya kwanza, mjini Mombasa, Nakuru na Machakos.

Mvua kubwa hasa mjini Machakos ilisabisha mchuano wa nusu fainali kati ya Kenya na Tanzania kuahirishwa kutokana mvua kubwa iliyoharibu uwanja wa soka wa Machakos.

Uganda waliokuwa mabingwa wa taji hili mwaka uliopita waliondolewa katika hatua ya robo fainali na Tanzania bara lakini wanasalia kuwa na rekodi nzuri ya kushinda mataji mengi ya CECAFA mara 13, iifuatwa na Kenya mara 6 na Ethiopia mara 4.

Kilimanjaro Stars ya Tanzania bara imewahi kutwaa ubingwa wa taji hili mara 3.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.