Pata taarifa kuu
SOKA

Serikali ya Nigeria yapanga kumlipa mshahara mnono kocha wa Super Eagles Stephen Keshi

Serikali ya Nigeria inapanga kuchukua hatua kumlipa mshahara mnono kocha wa timu ya taifa Stephen Keshi, waziri wa michezo ametangaza, na kuahidi kuwa italipa malimbikizo yote ya mishahara yake. 

Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi
Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi analysisfc.com
Matangazo ya kibiashara

Waziri wa michezo Bolaji Abdullahi amesema kuwa wamepokea kibali kutoka kwa Rais Goodluck Jonathan kuchukua madai ya mishahara ya Keshi na wasaidizi wake, ambaye anadai jumla ya Naira milioni 78 sawa na Euro 485,000,357,000

Keshi, ambaye analipwa kiasi cha naira milioni tano kwa mwezi, ingawa haijawahi kulipwa kwa takribani miezi mitano, aliiwezesha timu ya taifa ya Nigeria kushiriki michuano ya kombe la mataifa ya Africa na kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil.

Waziri wa michezo amewaambia waandishi wa habari kuwa ofisi ya rais inafanya mipango kwa ajili ya kumlipa Keshi malimbikizo ya mishahara yake yote.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.