Pata taarifa kuu
Michezo

Mwamuzi wa mchuano Manchester City na CSKA Moscow kuondolewa kibaruani baada ya kushindwa kudhibiti ubaguzi wa rangi

Mwamuzi aliyesimamia mchuano wa Manchester City dhidi ya CSKA Moscow ametakiwa kuondolewa kibaruani baada ya kushindwa kudhibiti tabia mbaya inayolalamikiwa katika viwanja vya michezo ya Ubaguzi wa rangi.

Kiungo mshambuliaji wa Man City Yaya Toure amelalamika kufuatia kelele za kejeli kutoka kwa mashabiki wa SCKA Moscow ya Urusi ambazo hazikuchukuliwa hatua yoyote na Mwamuzi wa mchuano.
Kiungo mshambuliaji wa Man City Yaya Toure amelalamika kufuatia kelele za kejeli kutoka kwa mashabiki wa SCKA Moscow ya Urusi ambazo hazikuchukuliwa hatua yoyote na Mwamuzi wa mchuano. RFI
Matangazo ya kibiashara

Kiungo mshambuliaji wa Man City Yaya Toure alilalamika Ovidiu Hategan kuhusu maneno ya kejeli za kiubaguzi wa rangi kutoka kwa mashabiki wa CSKA katika mchuano wa ligi ya mabingwa iliyofanyika nchini Urusi.

Mwamuzi huyo ametakiwa kuondolwa wadhifa huo kufuatia kushindwa kutekeleza jukumu lake usiku wa jumatano suala ambalo lipo wazi linapaswa kushughulikiwa na shirikisho la kandanda barani Ulaya,UEFA.

Sheria za mwaka 2009 za shirikisho la kandanda barani Ulaya UEFA ambazo zinatumika kuongoza mchezo huo zinampa mamlaka mwamuzi wa mchezo kushughulikia kejeli za ubaguzi wa rabgi kutoka kwa wafuasi.

Kwa hatua ya kwanza mchuano huweza kusimamishwa na kutoa onyo kwa watazamaji wote wanaofuatilia mchuano huo kwa wakati huo.

Hatua ya pili kwa mujibu wa sheria hiyo ni kuahirisha mchuano huo kwa muda mfupi ili kuona kama tabia hiyo imekoma ikiwa itaendelea hatimaye ni kufuta mchuano kabisa.

Mchuano huo uliisha kwa Manchester City kuibuka kwa ushindi wa bao 2-1 dhidi ya wenyeji SCKA Moscow.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.