Pata taarifa kuu
Michezo-Football

Black Stars ya Ghana yaicharaza bao 6 kwa 1 timu ya mafarao wa Misri

Timu ya taifa ya soka ya Ghana ya Black Stars imeicharaza bao 6 kwa 1 timu ya mafarao wa Misri katika uwanja wake wa nyumbani wa Babayarsa katika kutafuta tiketi ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil.

Kikosi cha timu ya soka ya Ghana wanatarajia kuumana na Misri mwezi ujao katika mchuano wa awamu ya pili
Kikosi cha timu ya soka ya Ghana wanatarajia kuumana na Misri mwezi ujao katika mchuano wa awamu ya pili
Matangazo ya kibiashara

Mabao ya Black Stars yalitiwa kimyani na mshambulizi matata Asamoah Gyan, huku shambulizi la Michael Essien likimsababisha Wael Gomaa kujifunga katika bao lake.

Mshambulizi wa Misri Mohamed Aboutrika aliipatia timu yake bao la pekee kupitia mkwaju wa Penalti na hadi kufikia kipindi hicho Ghana ilikuwa imepata mabao 3 kwa 1.

Mabao mengine ya Ghana yalifungwa na Sulley Muntari kupitia mkwaju wa Penalti, kabla ya Christian Atsu kuifunga Misri bao la 6 katika mchuano huo wa mzunguko wa kwanza.

Ushindi wa Ghana unaelezwa na wachambuzi wa soka kuwa haukutarajiwa na huenda mchuano wa mzunguko wa pili utakaochezwa mwezi ujao.

Mchuano huu ni muhimu sana kwa timu hizi mbili, Ghana kwa upande wake ikijaribu kufuzu katiika mashindano haya ya kombe la dunia kwa mara ya tatu mfululizo huku Misri nayo ikitaka kufuzu baada ya kufanya hivyo mara ya mwisho mwaka 1990.

Misri inastahili kushinda mchuano wa marudiano kwa kuifunga Ghana mabao 5 kwa 0 ili kufuzu katika kombe la dunia mwaka 2014.

Mchuano wa maruadiano utachezwa mwezi ujao, nchini Misri ikiwa shirikisho la soka duniani FIFA litakuwa limeridhika na hali ya usalama nchini humo, lakini chama cha soka nchini Ghana kinataka mchuano wa marudiano uchezwe nje ya taifa hilo kwa sababu za kiusalama.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.