Pata taarifa kuu
SOKA-GHANA

Shirikisho la soka nchini Ghana laomba FIFA kuhamisha mchuano wake kutoka Misri

Shirikisho la soka nchini Ghana linaiomba shirikisho la soka duniani FIFA kuhamisha mchuano wa marudiano wa kufuzu kwa kombe la duniani nchini Brazil dhidi ya Misri katika uwanja mwingine nje ya taifa la Misri kwa sababu za kiusalama.

Matangazo ya kibiashara

GFA kinasema kuwa kuna kinahofia usalama wa wachezaji wake kutokana na visa vya uvunjifu wa amani ambavyo vimeendelea kushuhudiwa katika nchi hiyo katika siku za hivi karibuni, hasa baada ya watu 50 kuuawa mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Cairo.

FIFA imepanga kuwa mchuano huo wa marudiano uchezwe tarehe 19 mwezi Novemba jijini Cairo, mji ambao uongozi wa soka nchini Ghana unasema kuwa hauna imani nao.

Mbali na kutokuwa na imani na mahali pa kuchezwa kwa mchuano huo, chama cha soka nchini Ghana kinasema kuwa kinawahofia pia mashabiki wa Misri ambao inaona wanaweza kuzua fujo uwanjani kama ilivyokuwa mwaka uliopita wakati wa mchuano wa ligi kuu nchini humo na kusabisha vifo vya zaidi ya mashabiki 70.

Ghana imeendelea kulalamika kuwa Misri imekuwa ikitumia uwanja wake wa nyumbani kucheza mechi kadhaa za kufuzu kushiriki katika kombe la dunia dhidi ya Msumbiji, Zimbabwe na Guinea bila ya mashabiki kufika uwanjani kwa hofu ya mashabiki kupigana jambo ambalo pia inasema linaweza kutokea.

FIFA inasema kuwa imepata ombi la Ghana na inafanya uchunguzi wake kabla ya kutoa mwelekeo kuhusu ikiwa mchuano huo uondolewe jijini Cairo au uendelee kuchezwa kama ilivopangwa.

Mchuano wa mzunguko wa kwanza wa kufuzu kwa kombe la dunia utachezwa mjini Kumasi tarehe 15 mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.