Pata taarifa kuu
SOKA-NIGERIA

Kocha Mkuu wa Nigeria Stephen Keshi asisitiza kuendelea na mkakati wake wa kujenga kikosi imara

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Nigeria Stephen Keshi ameweka wazi yupo kwenye harakati za kuendelea kuijenga Timu hiyo na hadi kufika sasa bado hajapata Kikosi ambacho anakihitaji.

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Nigeria Stephen Keshi akiwa kibaruani
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Nigeria Stephen Keshi akiwa kibaruani
Matangazo ya kibiashara

Keshi ambaye amefanikisha Nigeria kutwaa Ubingwa wa Kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2013 yaliyofanyika nchini Afrika Kusini kabla ya kukata tiketi ya kuingia hatua ya mtoano kusaka tiketi ya kucheza Kombe la Dunia hapo mwakani.

Kocha huyo aliyechukua nafasi ya Samson Siasia aliyeshindwa kuipeleka Nigeria kwenye mashindano ya AFCON ya mwaka 2012 amesema bado kuna safari ndefu sana kuhakikisha Nigeria inakuwa na kikosi bora kama ilivyozoeleka.

Keshi ameweka bayana atafanya kila linalowezekana bila kujali muda utakaotumika kuhakikisha anatengeneza timu itakayoleta mapinduzi ya soka ndani ya taifa hilo lililopoteza heshima yake katika siku za karibuni.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 51 amesema licha ya kupata kikosi alichonacho kwa sasa lakini hiyo siyo ishara ya kwamba mpango wake wa kutengeneza Kikosi imara umefikia ukingoni.

Keshi amesisitiza kuwa licha ya kupata mafanikio machache tangu aanza kuinoa Super Eagles lakini bado anakazi kubwa na ngumu ya kuhakikisha Nigeria inakuwa timu ya ushindani zaidi.

Licha ya kukabiliwa na panda shuka za mara kwa mara Keshi amesema malengo yake yatatimia na ndiyo itakuwa fahari kubwa kwa upande wake kuona amechangia kutengeneza Kikosi kilichobora.

Keshi amesisitiza ataendelea kutoa nafasi kwa wachezaji wachanga na wapya kila itakapoonekana kuna umuhimu wa kufanya hivyo akiamini hiyo ni njia mojawapo ya kuwa na kikosi kipana zaidi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Super Eagles ameweka bayana Nigeria inahitaji kuwa na wachezaji ambao wataisadia kupata matokeo mazuri yatakayokuwa sehemu ya mafanikio ya baadaye.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.