Pata taarifa kuu
MASHNDANO YA RIADHA YA DUNIA-URUSI

Baada ya mashindano ya riadha, Bingwa wa mita mia moja Usein Bolt apongeza maandalizi

Katika habari za michezo jioni ya leo tuanzie katika Michuano ya kimataifa ya Riadha kwa mwaka 2013 ambayo imekamilika jana jumapili mjini Moscow nchini Urusi ambapo Mjamaika Usain Bolt bingwa wa mbio za 100, amefaniukiwa kutetea ubingwa wake wa dunia wa mita 200 kwa muda wa sekunde 19 nukta 6.

Bingwa wa Dunia wa mita 100 na 200 Usein Bolt
Bingwa wa Dunia wa mita 100 na 200 Usein Bolt
Matangazo ya kibiashara

Mara baada ya kutamatika kwa michuano hiyo Bolt amewaambia mashabiki wake kwamba mashindano hayo yamekuwa ni mashindano ya tofauti, sio kuwa ni ya pekee sana, lakini, amesema anadhani kwa siku zote mashindano yameenda vizuri, watu walikuwa wamejiandaa, aa watu walikuwa wanatabasamu, kulikuwa na mashabiki wengi, kwa hiyo kwake yeye hilo limeniwezesha kupata ushindi kwa hiyo ameendelea ameweza kufikia malengo yangu.

kwa upande wa Kenya wao wanashangilia mafanikio ya Asbel Kiprop kwa upande wa wanaume wanaokimbia mita 1,500 na Eunice Sum kwa mbio za mita 800 wanawake, kwa maana hiyo Kenya ndiyo iliyoweza kuongoza kwa bara la Afrika katika michuano hiyo ya mwaka huu wa 2013

Mkenya Ezekiel Kemboi ambaye anashilikilia nafasi kama bingwa wa dunia wa mita 3000 alimaliza mchezo wake baada ya dakika 8 nukta 06 sekunde mbele ya Kipruto Conseslus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.