Pata taarifa kuu
SOKA-COPA LIBERTADORES

Klabu ya Atletico Mineiro ya Brazil ndiyo Mabingwa wapya wa Kombe la Copa Libertadores baada ya kuwafunga Olimpia

Klabu ya Atletico Mineiro ya nchini Brazil imefanikiwa kutwaa Kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Amerika Kusini baada ya kuwafunga wapinzani wao Olimpia ya kutoka Paraguay kwa mikwaju ya penalti 4-3. Atletico imefanikiwa kutwaa ubingwa huo wa Copa Libertadores baada ya kufanikiwa kushindi magoli 2-0 kwenye muda wa dakika 120 za mchezo huo lakini haikuwawezesha wao kutwa taji hilo hadi kwenye matuta.

Wachezaji wa Timu ya Atletico Mineiro wakishangilia Ubingwa wa Kombe la Copa Libertadores
Wachezaji wa Timu ya Atletico Mineiro wakishangilia Ubingwa wa Kombe la Copa Libertadores
Matangazo ya kibiashara

Olimpia ilifanikiwa kushinda mchezo wa kwanza kwa magoli 2-0 walipokuwa nyumbani Paraguay na walikuwa wanatakiwa kulinda ushindi huo ili watwae ubingwa wa Copa Libertadores lakini wakashindwa kufanya hivyo.

Mchezo huo ulilazimika kuamuliwa kwa matuta baada ya Atletico kupata ushindi wa magoli mawili kupitia kwa Jo aliyefunga katika dakika ya 36 kabla ya Leonardo Silva hajafunga goli la pili dakika tatu kabla ya mchezo haujaisha.

Klabu ya Atletico ikaibuka na ushindi kwenye mikwaju ya penalti kwa 4-3 kwenye mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Mineirao na kuhudhuriwa na mashabiki 60,000 kutoka Brazil na Paraguay.

Mchezaji wa zamani wa Barcelona, AC Milan na Paris Saint-Germain Ronaldo de Assis Moreira maarufu kama Ronaldinho alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wa Atletico waliofanikisha Klabu hiyo kutwaa taji la Copa Libertadores na mwenyewe amesema hiyo sababu iliyomfanya arejee Brazil.

Ronaldinho maarufu kwa jina la Gaucho amesema Klabu yake ya Atletico kutwaa taji hilo kumeonesha ni kwa namna gani yeye anaendelea kuisaidia timu iliyomsajili akitokea Barani Ulaya alikokuwa anachezea AC Milan.

Kocha Mkuu wa Atletico Ever Almeida amefurahishwa na hatua ya Klabu yake kuibuka na taji hilo lakini amekiri walipoteza nafasi nyingi za magoli kitu ambacho si kizuri kwenye mchezo wa fainali.

Atletico Mineiro imekata tiketi ya kuliwakilishi Bara la Amerika Kusini kwenye mashindano ya Kombe la Dunia la Klabu zitakazofanyika nchini Morocco mwezi Desemba huku Amerika Kaskazini ikiwakilishwa na Monterrey huku Bayern Munich akiwa binga wa Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.