Pata taarifa kuu
MICHEZO

Mali yajikusanyia alama baada ya kutoka sare na Paraguay.

Mali imafanikiwa kutoka sare ya bao moja kwa moja katika mechi ya ufunguzi ambayo ilizikutanisha Mali na Paraguay,michuano ya kufuzu kushiriki kombe la dunia,mchuano huo ulifanyikia Gaziantep, nchini Uturuki jumamosi.

Kikosi cha Mali ambacho kiliibuka sare ya bao 1-1 katika mchuano wake dhii ya  Paraguay
Kikosi cha Mali ambacho kiliibuka sare ya bao 1-1 katika mchuano wake dhii ya Paraguay facebook.com
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji nyota Adama Niane alifungua pazia kwa kuzifumania nyavu baada ya dakika tatu za mchezo huku shangwe hizo zikidumu kwa dakika chache kabla ya Jorge Rojas kuisawazishia goli timu ya Amerika kusini Paraguay.

Timu hiyo kutoka barani Afrika inapata alama ya kwanza ya michuano baada ya kupoteza katika ufunguzi mnamo mwaka 2009 kwa mabingwa Ghana na Nigeria.

Katika michuano hiyo mabingwa wa Ghana walipoteza kwa Ufaransa kwa ipigo cha 3-1 huku Nigeria ikichapwa 3-2 na Wareno.

Mabingwa wa Afrika Misri watafungua kampeni hizo dhidi ya Chile jumatatu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.