Pata taarifa kuu
UGANDA-LIBERIA

Beki wa Kushoto wa Uganda Godfrey Walusimbi huenda akaukosa mchezo dhidi ya Liberia utakaopigwa siku ya jumamosi

Timu ya taifa ya Uganda maarufu kwa jina la Cranes huenda ikamkosa beki wake wa kutumainiwa wa kushoto Godfrey Walusimbi kwenye mchezo wao wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka 2014 nchini Brazil dhidi ya Liberia. Walusimbi ameondoka kwenye kambi ya Timu ya Taifa ya Uganda iliyopo Uwanja wa Namboole kutokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia licha ya kwamba kiwango chake pia kinatajwa kushuka.

Beki wa Kushoto wa Uganda Godfrey Walusimbi akipambana na Mshambuliaji wa Tanzania Mrisho Ngasa
Beki wa Kushoto wa Uganda Godfrey Walusimbi akipambana na Mshambuliaji wa Tanzania Mrisho Ngasa
Matangazo ya kibiashara

Beki huyo wa kushoto aliyejiunga na timu ya Don Bosco ya nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kabla ya kuachwa bila ya sababu zozote zilizoanishwa juu ya uamuzi huo.

Walusimbi hakuwepo kwenye mchezo ambao Cranes ilipata kichapo cha magoli 2-0 mbele ya Liberia mchezo uliopigwa mwezi Machi kutokana na kuwa mgonjwa lakini sasa anakosa mchezo wa marudiano.

Kocha Mkuu wa Cranes Milutin Micho Sredojevic amekiri Walusimbi ni beki bora wa kushoto Barani Afrika lakini kwa sasa hayupo sawa kuweza kuchezo mchezo dhidi ya Liberia utakaopigwa siku ya jumamosi.

Micho amesema wanaendelea kufuatia mambo yanayomkabili Walusimbi kabla hawajafikia uamuzi wa kumtumia au kumuacha kwenye kikosi cha Cranes lakini nafasi yake inaweza ikachukuliwa na Joseph Ochaya anayecheza Asante Kotoko.

Meneja Habari wa Cranes Fred Katende Malibu amesema Walusimbi amelazimika kuondoka kwenye kambi kutokana na mkewe kusumbuliwa na mardhi yaliyomfanya alazwe kabla ya kuruhusiwa kutoka Hospital siku ya jumatano na yeye ndiye anamuangalia kwa karibu.

Katika hatua nyingine wapinzani wa Cranes ambao ni Liberia wamejigamba kuhakikisha wanachukua ushindi kwenye mchezo wao wa jumamosi ili kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa Kombe la Dunia mwaka 2014.

Mchezaji wa Bora wa Dunia na Ulaya wa zamani George Weah ambaye yupo na kikosi cha Liberia kinachonolewa na Kocha Nagbe Jericho ndiye ambaye amesema wanauhakika wa kuibuka na ushindi.

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Liberia kinaendelea na mazoezi yake kwenye Uwanja wa Nakivubo kabla ya mtanange wao dhidi ya Uganda utakaopigwa siku ya jumamosi kusaka tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2014.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.