Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Everton yakubali kulipa fidia kwa Wigan Athletic ili kuweza kumpata Roberto Martinez anoe kikosi chao

Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imekubaliana na wenzao wa Wigan Athletic kuwalipa fidia kutokana na kumchukua Kocha wao Mkuu Roberto Martinez ambaye anatarajiwa kuingia mkataba wa kuwanoa Toffees msimu ujao. Martinez anatarajiwa kuchukua mikoba iliyoachwa na David Moyes aliyekwenda kujiunga na Manchester United kwa lengo la kuinoa timu hiyo msimu ujao baada ya Sir Alex Ferguson kutangaza kustaafu wadhifa wake.

Roberto Martinez Kocha wa zamani wa Wigan Athletic ambaye anasakwa na Everton
Roberto Martinez Kocha wa zamani wa Wigan Athletic ambaye anasakwa na Everton www.ddwt.me.uk
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Klabu ya Wigan Dave Whelan amethibitisha kufikia makubaliano na wenzao wa Everton kupitia Mwenyekiti mwenzake Bill Kenwright ili kupata fidia hiyo kutokana na kuvunjwa mkataba wa kocha wao.

Whelan ameweka bayana kwa sasa Martinez yupo huru kufanya mazungumzo na Everton na wakiafikiana anaweza kuingia mkataba wa kuinoa timu hiyo baada ya wao kumalizana naye kutokana na kupewa fidia.

Makubaliano hayo yanatoa nafasi kwa Martinez kuanza mazungumzo ambayo yanamfanya aweze kurithi nafasi ya Moyes huku akiwa na rekodi ya kutwaa Kombe la Chama Cha Soka nchini Uingereza FA.

Martinez mwenye umri wa miaka 39 ameweza kuipa Wigan ubingwa baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa muda mrefu kitu ambacho kimemfanya thamani yake kuongezeka na Everton kuona anafaa kuwa mrithi wa Moyes.

Taarifa kutoka ndani ya Klabu ya Everton zimeeleza hii leo inaweza ikamtangaza rasmi Martinez kuwa Kocha Mkuu wa Timu hiyo kwa mkataba ambao utabainishwa baada ya kufikia makubaliano baina ya pande hizo mbili.

Martinez alijiunga na Wigan Athletic akitoka Klabu ya Swansea mwezi Juni mwaka 2009 na alikuwa anawindwa na Aston Villa mwaka 2011 kabla ya Liverpool hajaonekana kumhitaji ambapo alikataa ofa zote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.