Pata taarifa kuu
TENNIS-FRENCH OPEN

Roger Federer atinga Robo Fainali ya Mashindano ya French Open baada ya kumfunga Gilles Simon

Mchezaji Tennis nambari mbili kwa ubora upande wa Wanaume Roger Federer amefanikiwa kusonga mbele kwa kumfunga Gilles Simon kwa seti tatu kwa mbili katika mchezo ambao almanusura ushuhudie raia huyo wa Uswiss akaondolewa mapema katika Mashindano ya French Open.

Roger Federer akishangilia baada ya kumfunga Gilles Simon kwenye Mashindano ya French Open
Roger Federer akishangilia baada ya kumfunga Gilles Simon kwenye Mashindano ya French Open
Matangazo ya kibiashara

Federer amefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya mashindano ya French Open baada ya kufanikiwa kupambana vilivyo kutoka nyuma baada ya kufungwa seti mbili kwa moja na hatimaye kuweza kushinda seti mbili za mwisho na kupata ushindi.

Mchezaji huyo ambaye ameshashinda Taji la French Open alinusurika kuondolewa mapema katika mashindano hayo kama ilivyomkuta mwaka 2004 kutokana na kupambana vilivyo na kujipatia tiketi ya Robo Fainali.

Federer alianza vizuri mchezo huo baada ya kushinda seti ya kwanza kwa 6-1 kabla ya Mpinzani wake Simon hajazinduka usingizini na kushinda seti mbili mfululizo kwa 4-6 na 2-6 na kumfanya aongoze.

Simon baada ya kushinda seti hizo mbili kulimfanya Federer azinduke kutoka usingizini na hatimaye kufanikiwa kucheza kwa makini zaidi na kushinda seti mbili mfululizo kwa 6-2 na 6-3 na hivyo kutinga Robo Fainali.

Ushindi huo wa Federer umemfanya aweze kuweka rekodi nzuri ya kushinda michezo 900 katika mashindano makubwa ya Tennis huku akiahidi kupigana na kutwaa Taji la French Open mwaka huu.

Michezo mingine ya mzungumzo wa nne imeshuhudia Tommy Robredo akitinga Robo Fainali baada ya kumfunga Nicolas Almagro kwa seti tatu kwa mbili kwa matokeo ya 6-7, 3-6, 6-4, 6-4 na 6-4.

Jo-Wilfried Tsonga naye ametinga Robo Fainali ya Mashindano ya French Open kwa kumfunga Viktor Troicki kwa seti tatu kwa bila kwa 6-3, 6-3 na 6-3 huku David Ferrer akifuzu kwa kumfunga Kevin Anderson kwa 6-3, 6-1 na 6-1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.