Pata taarifa kuu
MPIRA WA MIGUU

Benitez atangazwa kocha mpya wa FC Napoli ya Italia

Klabu ya Napoli ya nchini Italia inayoshiriki ligi kuu ya Seria A, imemtangaza aliyekuwa kocha wa muda wa Chelsea, Rafa Benitez kama kocha mkuu mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Walter Mazzarri aliyejiunga Inter Milan.

Kocha Rafa Benitez anayechukua mikoba kuifundisha klabu ya Napoli ya Italia
Kocha Rafa Benitez anayechukua mikoba kuifundisha klabu ya Napoli ya Italia Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema kuwa Benitez amesaini mkataba wa miaka miwili kukinoa kikosi hicho ambacho kitashiriki michuano ya klabu bingwa ulaya msimu ujao baada ya kumaliza kwenye nafasi ya pili nyuma ya Juventus.

Wakati akiwa kocha wa muda na klabu ya Chelsea, Benitez aliwezesha timu hiyo kutwaa taji la Europa na kufanikiwa kumaliza kwenye nafasi ya tatu katika ligi kuu ya nchini Uingereza na kuihakikishia timu hiyo kushiriki klabu bingwa ulaya msimu ujao.

Akiwa na Chelsea, Benitez pia alifanikiwa kuifikisha fainali ya klabu bingwa ya dunia nchini Japan na kufungwa na timu ya Corithians ya nchini Brazil.

Benitezi alijiunga na Chelsea kuchukua mikoba ya kocha Roberto Di Matteo ambapo wakati akianza kibarua chake alikutana na upinzani mkali toka kwa mashabiki wa Chelsea ambao walikuwa hawamtaki.

Kocha wa Real Madrid Josee Mourinyo anahusishwa kujiunga tena na klabu hiyo.

Kocha huyu pia amewahi kuvifundisha vilabu vya Valencia, Liverpool na Inter Milan ambapo sasa anarejea tena nchini Italia baada ya kutokuwepo nchini humo kwa karibu miaka 8.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.