Pata taarifa kuu
UINGEREZA-SOKA

Manchester United kumpa David Moyes mkataba wa miaka sita kuinoa timu hiyo kurithi mikoba ya Sir Ferguson

Klabu ya Manchester United imefanikiwa kumtangaza mrithi wa Sir Alex Ferguson aliyetangaza kustaafu kazi ya kukinoa kikosi hicho mwishoni mwa msimu huu baada ya kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka 26.

Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwa na mrithi wake David Moyes
Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwa na mrithi wake David Moyes
Matangazo ya kibiashara

Manchester United imemtangaza David Moyes aliyekuwa anainoa Everton kuwa ndiyo kocha mpya wa Mashetani hao Wekundu ambapo atasaini mkataba wa miaka sita ifikapo tarehe mosi ya mwezi Julai.

Sir Ferguson ndiye alitangaza kufikiwa kwa makubaliano baina ya Bodi ya Wakurugenzi wa Manchester United na Moyes ili aweze kuwa mrithi wake hapo Old Trafford kunzia msimu ujao.

Moyes mwenye umri wa miaka 50 anaondoka Goodison Park baada ya kuifundisha Everton kwa kipindi cha miaka 11 bila ya kuipa taji lolote huku kitu pekee ambacho anasifiwa kukifanya na kutengeneza kikosi imara.

Sir Ferguson ndiye alimpendekeza Moyes kuwa mrithi wake ambapo mwenyewe amemsifu ni kocha imara mwenye vigezo vyote vinavyopaswa kuweza kuinoa Manchester United kwa siku zijazo.

Moyes mwenyewe baada ya kutangazwa kuwa mrithi wa Sir Ferguson amekiri hiyo ni heshima kubwa sana kwake na anashukuru kwa kupewa kazi hiyo na ameahidi kuhakikisha anailetea mafanikiwa Manchester United.

Klabu ya Everton imetoa taarifa yake ya kumshukuru Moyes kwa kazi aliyoifanya kwa kipindi cha miaka 11 aliyokuwa anaifundisha timu hiyo huku wakimtakia kila la kheri katika kazi yake mpya.

Beki wa Kati wa Manchester United Rio Ferdinand ni miongoni mwa waliouzungumziaujio wa Moyes ambapo yeye amesema kuna vitu ambavyo analingana na Sir Ferguson hivyo ana imani atakuwa na mafanikio Old Trafford.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.