Pata taarifa kuu
UINGEREZA-michezo

Kumi washikiliwa na polisi kuhusika na vurugu katika michuano ya nusu fainali za kombe la FA.

Watu kumi wanashtakiwa kuhusika na vurugu zilizotokea baina ya mashabiki wa millwall katika michuano ya nusu fainali ya kombe la FA ambapo klabu ya daraja la chini Millwall ya nchini Uingereza ilicheza dhidi ya Wigan.

Roberto Martinez kocha mkuu wa Wigan akifurahia ushindi wa timu yake
Roberto Martinez kocha mkuu wa Wigan akifurahia ushindi wa timu yake Reuters
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi cha pili baada ya kufungwa bao mbili bila takribani mashabiki 20 wa millwall walikabiliana wenyewe katika uwanja wa Wimbley.

Tukio hilo ambalo halikupendeza machoni pa wengi lilishuhudiwa na mamilioni ya mashabiki wa soka kupitia luninga lilisababisha baadhi ya mashabiki ambao mchezo wa kandanda upo damuni na wengine chipukizi kutokwa machozi.

Alex Horne, ambaye ni katibu mkuu wa FA alisema jeshi la polisi sambamba na shirikisho la kandanda nchini humo linafanya uchunguzi kubaini ukiukwaji wa sheria na utovu wa nidhamu uliofanywa siku ya michuano ya kombe la FA ili kubaini wahusika wote na kuchukuliwa hatua za kisheria.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.