Pata taarifa kuu
SOKA-UINGEREZA

Kocha wa Manchester United Alex Ferguson amtaka Mshambuliaji Van Persie kurejesha makali yake ya ufungaji

Kocha Mkuu wa Klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson amemgeukia Mshambuliaji wa Kimataifa wa Uholanzi anayekipiga katika timu yake Robin Van Persie kutokata tamaa licha ya kucheza micheo tisa bila ya kufunga goli. Ferguson amemtaka Mshambuliaji wake kutobweteka na magoli ambayo amefunga na badala yake aongeze juhudi kuhakikisha anarudi katika kiwango chake ambacho alikuwa anafunga magoli katika kila mechi hapo kabla.

Mshambuliaji wa Manchester United Robin Van Persie akiwa mazoezini
Mshambuliaji wa Manchester United Robin Van Persie akiwa mazoezini
Matangazo ya kibiashara

Kocha huyo amesema Van Persie hapaswi kupumzika kwa namna yoyoye ile kwa kuwa amekuwa madhubuti na anatakiwa kuongeza juhudi na umakini anapokuwa uwanjani ili kuendelea kufunga mfululizo.

Ferguson ameeleza kuna kipindi kila mshambuliaji huwa anapitia wakati mgumu na kukabiliwa na uhaba wa magoli lakini hiyo si sababu ya kujiona huwezi kurejea kwenye kiwango chao cha kawaida.

Van Persie aliyenunuliwa kutoka Klabu ya Arsenal kwa kitita cha pauni milioni 24 amefunga magoli 23 katika michezo 31 aliyoichezea Manchester united kwenye michezo yote ya mashindano.

Mshambuliaji huyo anashinda nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora nchini Uingereza akiwa na magoli 19 nyuma na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez ambaye amefunga magoli 22.

Ferguson amesisitiza huu ni wakati wa Van Persie kuendelea kuonesha makali yake kukiwa kumesalia michezo nane kabla ya Ligi Kuu kufikia tamati na Manchester United wakisaka taji lao la 20 kwa udi na uvumba.

Ferguson pia amezungumzia hali ya majeruhi katika kikosi chake ambapo amesema Wayne Rooney na Rafael Da Silva wameanza mazoezi na hivyo wanaweza wakawepo kwenye mchezo wa jumatatu dhidi ya Manchester City utakaopigwa Old Trafford.

Kocha huyo amesema mabeki wawili wa kati ambao ni nahodha Nemanja Vidic na Jonny Evans huenda wasiwepo kwenye kikosi chake kutokana kuwa kwenye hati hatia sababu bado hawajayashinda maumivu.

Manchester United inaongoza Ligi Kuu nchini Uingereza ikiwa na pointi kumi na tano zaidi dhidi ya wapinzani wake Manchester City wanaoshikilia nafasi ya pili na wanatarajiwa kupambana usiku wa jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.