Pata taarifa kuu
UEFA

Manchester United yapata sare ya bao 1 kwa 1 dhidi ya Real Madrid mchuano wa UEFA

Manchester United ya Uingereza ilitoka sare ya bao 1 kwa 1 na Real Madrid ya Uhispania katika mchuano wa timu kumi na sita bora kuwania taji la klabu bingwa barani Ulaya UEFA.

Matangazo ya kibiashara

Danny Welbeck wa Manchester United aliwapa vijana wa Sir Alex Ferguson uongozi katika mchuano huo kipindi cha kwanza kupitia shambulizi la kichwa baada ya kupokea kona murua kutoka kwa mshambulizi matata Wayne Rooney.

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Christiano Ronaldo aliisawazishia Real Madrid kabla ya wakati wa mapumziko.

Timu zote zilipoteza nafasi nyingi za kupata mabao katika mchuano huo mgumu ulioelezwa na kocha wa Real Madrid kuwa ndio mechi iliyokuwa inasubiriwa kutazamwa na mashabiki wa soka duniani.

Bao la Christiano Ronaldo lilikuwa la 35 katika mechi 34 alizocheza msimu huu, na kwa mujibu wa shirikisho la soka barani Ulaya UEFA aliongoza katika ushambulizi huku akipata mashuti 10 manne yakilenga goli huku Robin Van Persie akiongoza upande wa Manchester United na kulenga goli mara nne.

Real Madrid na Manchester United sasa zitakutana  katika duru ya pili ya michuano hiyo tarehe 5 mwezi wa Machi katika uwanja wa Old Trafford nchini Uingereza mchuano ambao kocha wa Madrid Jose Mourinho amesema utaonyesha thamani yake katika klabu hiyo na soka la Uhispania.

Mourinho ambaye amewahi kuiongoza klabu ya Porto na Inter Milan kushinda taji hili la UEFA amesema vijana wake wana uwezo wa kuifunga Manchester United katika uwanja wao wa nyumbani jambo analosema timu zingine zimewahi kufanya katika siku zilizopita.

Naye kocha wa United Alex Ferguson amesema amefurahishwa na sare hiyo huku akisifu juhudi zilizoonyeshwa na kipa David De Gea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.