Pata taarifa kuu
AUSTRALIA OPEN 2013

Li na Sharapova watinga hatua ya nusu fainali upande wa wanawake, wakati David Ferrer akifufua ndoto za kufika fainali ya michuano ya mwaka huu

Michuano ya tenesi ya Australia Open imeendelea kutimua vumbi nchini humo kwa magwiji wa mchezo huo kujikatia tiketi za kufuzu hatua ya nusu fainali.

David Ferer akishangilia ushindi alioupata hapo jana
David Ferer akishangilia ushindi alioupata hapo jana Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kwa upande wa wanawake mchezaji nambari 6 kwa ubora wa mchezo huo Li Na amefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kumfunga Agnieszka Rwadanscar kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 7-5 na 6-3.

Katika mchezo mwingine Maria Sharapova alifanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali kwa kumfunga Ekaterina Makarova kwa seti mbili bila kwa matokeo ya 6-2 na 6-2.

Kwa upande wa wanaume David Ferrer alifanikiwa kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali baada ya kumfunga Nicolas Almagro kwa seti 4-6, 4-6, 7-5 na 5-4 na hivyo kutinga hatua ya nusu fainali.

Roger Feder alifanikiwa kusonga mbele kwenye michuano hiyo baada ya kumfunga Milos Raonic kwa seti 4-6, 7-6 na 6-2, wakati Andy Murray yeye akisonga mbele kwa kumfunga Gilles Simon.

Baadae Novack Jokovich atacheza na Thomas Berdiyich wakati Jeremy Chardy atacheza na Andy Murray kwenye hatua ya robo fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.