Pata taarifa kuu
TENNIS

Roger Federer ampasha chipukizi wa mchezo huo Bernard Tomic

Nyota wa mchezo wa tennis Roger Federer raia wa Uswisi amemuonya chipukizi wa mchezo huo toka nchini Australia Bernard Tomic kuwa kuingia katika orodha ya wachezaji kumi bora duniani sio kazi rahisi kama yeye anavyodhani.

REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Federer amesema Tomic anatakiwa kukumbuka kuwa kuingia kumi bora ni hatua kubwa sana hivyo anahitaji juhudi za ziada ili aweze kuifikia nafasi hiyo.

Tomic aliyejitwalia ubingwa wa nane baada ya kushinda seti 6-3, 6-7(2/7), 6-3 dhidi ya Kevin Anderson katika fainali za kimataifa za Sydney jana jumamosi, alijigamba kuwa anaamini ataingia katika orodha ya wachezaji kumi bora duniani mwishoni mwa mwaka huu.

Kwa upande wake Tomic amesema Federer anafanya makosa kufikiria mustakabali wa wachezaji wengine wakati hata yeye mwenyewe bado anatakiwa kujiimarisha zaidi ili kutetea ubingwa wake.

Tomic mwenye umri wa miaka ishirini anatamani kushuka dimbani na Federer katika awamu ya tatu, na anaamini mchezo ni matokeo hivyo yeyote yule anaweza kuibuka na ubingwa.

Federer amepania kutwaa ubingwa kwa mara ya tano katika michuano ya wazi ya Australia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.