Pata taarifa kuu
ITALIA

Ubaguzi wa rangi wasababisha mchezo wa kirafiki kati ya AC Milan na Pro Patria uvunjike

Vitendo vya Ubaguzi wa rangi ambavyo vimefanywa na mashabiki wa Klabu ya Pro Patria ya nchini Italia kwenye mchezo dhidi ya AC Milan vimesababishwa kuvunjika kwa mchezo huo huku wachezaji weusi wakionekana kukasirishwa na kitendo hicho.

Mshambuliaji wa zamani wa Kimataifa wa Ghana ambaye anacheza katika Klabu ya AC Milan Kevin-Prince Boateng ambaye amekumbana na ubaguzi wa rangi kwenye mchezo wa kirafiki
Mshambuliaji wa zamani wa Kimataifa wa Ghana ambaye anacheza katika Klabu ya AC Milan Kevin-Prince Boateng ambaye amekumbana na ubaguzi wa rangi kwenye mchezo wa kirafiki
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa AC Milan wakiongozwa na Kevin-Prince Boateng ambaye alivua shati na kisha kupiga mpira upande wa mashabiki waliokuwa wanafanya ubaguzi wa rangi na kishwa kufuatwa na wachezaji wengine weusi.

Shirikisho la Soka Nchini Italia FIGC limetangaza kufanya uchunguzi kubaini wale ambao wamehusika kwenye kufanya vitendo hivyo vya kibaguzi ambavyo vimechangia kuvunjika kwa mchezo huo.

Mchezo huo ulivunjika katika dakika ya 25 baada ya Boateng kuchukizwa na maneno ya kibaguzi ambayo yalikuwa yanatolewa dhidi yake na wachezaji wengine weusi hatua iliyomfanya awapige mashabiki hao na mpira.

Boateng baada ya kufanya hivyo akavua jezi yake na kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia mavazi na kufuatwa na wachezaji wengine ambao walikuwepo uwanjani na baada ya muda mchezo huo ukavunjwa.

Wachezaji wengine weusi wa AC Milan ambao walikumbana na ubaguzi huo wa rangi kutoka kwa mashabiki wa Klabu ya Pro Patria ni pamoja na M'Baye Niang, Urby Emanuelson na Sulley Muntari.

Kocha Mkuu wa AC Milan Massimiliano Allegri baada ya kuvunjika kwa mchezo huo akawaambia wanahabari wamechukizwa mno na kitendo kilichofanywa na mashabiki wa klabu ya Pro Patria.

Licha ya juhudi kubwa kufanywa Barani Ulaya kuhakikisha vitendo vya ubaguzi vinamalizwa michezoni lakini kwa baadhi ya mashabiki wa mpira wa miguu wamekuwa hawaliewi hilo na badala yake wamekuwa mstari wa mbele kutekeleza hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.