Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Kocha Ferguson ataka wachezaji wa Manchester United kuendelea kucheza kwa kiwango chao cha sasa mwakani

Kocha Mkuu wa Vinara wa Ligi Kuu nchini Uingereza Manchester United Sir Alex Ferguson ana matumaini wataendelea na wimbi kupata matokeo mazuri kwenye Ligi Kuu pale watakaposhuka dimbani tarehe mosi ya mwezi January mwaka 2013 kupambana na Wigan Athletic.

Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwa anafuatilia mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza
Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguson akiwa anafuatilia mchezo wa Ligi Kuu nchini Uingereza
Matangazo ya kibiashara

Ferguson amekiri kiwango ambacho kinaoneshwa na wachezaji wake na kufanikiwa kushinda michezo mitano kati ya sita ambayo wamecheza katika kipindi cha mwezi wote wa Desemba na kuwa mbele ya wapinzani wao Manchester City kwa pointi saba.

Manchester United imefanikiwa kufunga magoli hamsini kwenye michezo yake ishirini ambayo wamecheza kitu ambacho kimeonesha amekuwa na washambuliaji wakali kwenye Ligi Kuu nchini Uingereza.

Ferguson ameonekana kukoshwa zaidi na matokeo ya ushindi wa nyumbani wa magoli 2-0 mbele ya West Bromwich Albion hivyo amewataka wachezaji wao kuhakikisha wanaendeleza kiwango walichonacho ili waweza kutwaa taji la 20.

Manchester United inakabiliwa na michezo baina ya Liverpool, Tottenham Hotspur, Southampton, Fulham na Everton kwenye kipindi cha majuma sita huku pia wakitarajiwa kukabiliana na Real Madrid kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Ferguson amekiri watakuwa na michezo migumu lakini anamatumaini walinzi wake Phil Jones na Rafael Da Silva watarejea kukisaidia kikosi chake kitu ambacho kitasaidia kupumzishwa kwa baadhi ya wachezaji wengine.

Huenda Ferguson akalazimika kumpumzisha Nemanja Vidic kwenye mchezo huo dhidi ya Wigan kutokana na mchezaji huyo kurejea baada ya kuwa majeruhi na inaweza ikawa vigumu kwake kucheza michezo miwili katika siku nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.