Pata taarifa kuu
Michezo-Football

Alex Furgason amfananisha Van Persie na Eric Cantona

Kocha wa Manchester United Sir Alex Furgason amesikika akimzungumzia mshambuliaji wa timu yake muholanzi Robin Van Persie na kumfananisha na Mfaransa aliewahi kuichezea timu hiyo Eric Cantona na kwamba anaweza pia kuandika Historia kama ilivyokuwa kwa mchezaji huyo ambae sasa amestafu kucheza soka.

Robin Van Persie wakati aliposaini kuichezea Man United akitokea Arsenal
Robin Van Persie wakati aliposaini kuichezea Man United akitokea Arsenal
Matangazo ya kibiashara

Furgason amesema kwamba Van Parsie anaouwezo kama ule aliokuw anao Cantona wakati alipojiunga na Klabu hiyo.

Van Persie amejiunga na Manchester United akitokea katika Klabu kubwa ya Arsenal alioichezea kuanzia mwaka 2004 hadi 2012 na kuendelea kujizatiti kushika kwenye nafasi yake.

Sir Alex Furgason ameendelea kuwa Van Persie mwenye umri wa miaka 29 amefunga mabao 31 kagika mechi 71 akiwa na timu yake ya taifa ya Uholanzi ambapo alijiunga na Manchester United baada ya kukipiga Arsenal kwa kipindi cha miaka 8 huku akiongozxa kama mfungaji bora wa ma bao.

Upande mwingine Furgason amesema Eric Cantona amekipiga katika Klabu hiyo kwa misimu mitano na kuipatishia Kombe Klabu ya mashetani weusi. 'The King Eric 'aliifungua Manchester united mabao 82 wakati akikipiga katika timu hiyo
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.