Pata taarifa kuu
UGANDA

Zanzibar Heroes yashindwa kutamba mbele Eritrea, yatoka suluhu

Mashindano ya Chalenji ya CECAFA yanaendelea nchini Uganda huku leo mchezo wa kwanza ulizikutanisha timu ya Zanzibar Heroes na Eritrea.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ya mchezo huo yamekuwa ni suluhu baada ya timu hizo kushindwa kunfangana katika vipindi vyote viwili.

Mchezo huo ulikuwa wa vuta nikuvute huku Eritrea wakikakamaa na kuonyesha uwezo tofauti na mara nyingine ambapo timu imekuwa akiambulia kubugizwa kapu la magoli.

Hata hivyo timu zote zilionyesha udhaifu katika umaliziaji kutokana na nafasi ambazo walikua wakizipata na kushindwa kuzitumia inavyotakiwa.

Kwa matokeo hayo timu hizo zinaonekana kuanza mashindano hayo kwa mwendo wa kinyonga na zikielekeza nguvu katika michezo mingine ijayo ya kundi C.

Mchezo mwingine wa leo Rwanda wanaonyeshana ubabe na timu ya Malawi ambayo imealikwa katika mashindano hayo.

Hiyo jana Timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars ilifanikiwa kuwachapa Sudan kwa bao 2-0 wakati Burundi iliyaanza kwa kishindo mashindano hayo baada ya kuivuruga Somalia kwa bao 5-1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.