Pata taarifa kuu
LONDON-UINGEREZA

Novak Djokovic na Roger Federer uso kwa uso

Mchezaji namba moja wa dunia katika mchezo wa tenisi Novak Djokovic hii atakuwa na kibarua kigumu atakapobiliana na mchezaji mahiri wa mchezo huo Roger Federer. 

RFI
Matangazo ya kibiashara

 

Miamba hao wawili wanakutana katika mchezo wa fainali za mashindano ya tenisi ya World Tour usiku wa leo huku mashabiki wa mchezo huo wakisubiri kwa hamu nani ataibuka mbabe katika mtanange huo.

Mchezo huo utakaopigwa jijini London nchini Uingereza utakua wa vuta nikuvute kwa kuwa wachezaji hao wanakaribiana viwango kwa karibu sana.

Novak Djokovic kwa upande wake yeye anaona ushindi kwake ni muhimu kwa sababu huo ni mchezo wake wa mwisho katika msimu huu.

Mchezaji huyo amesema kuwa atacheza kufa kupona ili kuutia kwapani ubingwa wa mashindano hayo ya mchezo wa tenisi.
Mchezaji huyo atashuka katika dimba la O2 Arena kwa mara ya kwanza tangu 2009 ambapo mashindano hayo yalihamishiwa huko London nchini Uingereza.

Roger Federer kwa upande wake anauona mchezo huo kuwa muhimu na ni vema akaondoka na ushindi na ameapa kutumia maarifa zaidi ili kuudhihirishia ulimwengu kuwa ana uwezo mkubwa.

Hata hivyo novak djokovic atamaliza mwaka huu akishikilia nambari moja katika ubora hata kama atapoteza mchezo wa leo kati yake na Roger Federer.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.