Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Wenger awasihi mashabiki wa Arsenal kumpa heshima Van Persie watakapoelekea Old Trafford

Kocha Mkuu wa Arsenal Arsene Wenger amewasihi mashabiki wa Klabu yake kutofanya vitendo vya kumdhihaki Mshambuliaji wa zamani wa Timu hiyo Robin Van Persie katika mchezo wao dhidi ya Manachester United utakaopigwa kesho.

Kocha Mkuu wa Arsenal Arsene Wenger akiwa na mshambuliaji wa zamani wa Klabu hiyo Robin Van Persie
Kocha Mkuu wa Arsenal Arsene Wenger akiwa na mshambuliaji wa zamani wa Klabu hiyo Robin Van Persie
Matangazo ya kibiashara

Wenger amewaasa mashabiki wa Arsenal kuhakikisha wanaonesha heshima kwa mchezo huyo ambaye ameitumikia timu hiyo kwa kipindi cha miaka nane kabla ya kuuzwa kwa kitita cha £24 milioni.

Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema Van Persie kwa kipindi cha miaka nane ameweza kutoa mchango mkubwa kwa Arsenal hivyo anastahili heshima ya kipekee badala ya mashabiki kumdhihaki na kumzomea.

Wenger ametoa kauli hiyo wakati huu Arsenal ikijiandaa kushuka katika Dimba la Old Trafford kukabiliana na Manchester United huku wakiwa na kumbukumbua mbaya ya kupata kichapo katika mchezo wa mwisho cha magoli 8-2.

Mfaransa huyo amewataka mashabiki wa Arsenal kukubaliana na hali halisi ya kuondokewa na Van Persie ambaye katika kipindi chake cha miaka nane ameweza kufunga magoli 132 kwenye michezo 281.

Kocha Mkuu wa Manchester United Sir Alex Ferguso amesema haamini kama mashabiki wa Arsenal ambao wataelekea Old Trafford watampa mapokezi mabaya Van Persie kutokana na kufanya mambo makubwa akiwa Emirates.

Van Persie ambaye alifunga magoli 44 katika michezo 57 aliyocheza msimu uliopita alikuwa ni mhimili wa safu ya ushambuliaji ya Arsenal lakini alionekana kuchoshwa na klabu hiyo kuendelea kukosa mataji.

Arsenal walitumia kitita cha £2.75m kumsajili Robin Van Persie akitokea Feyenoord mwaka 2004 ambapo aliweza kuwasidia kutokana na makali yake ambayo aliyaonesha tangu atue Highbury.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.